Kitu ambacho mashabiki wengi wa Music Tanzania
na hata nje ya Nchi wangependa kusikia kinaweza
kikawa kimekaribia, Meneja wa Diamond, Salaam
amepiga picha ya Pamoja na mpinzani mkubwa wa
msanii wake, Alikiba.
Haijajulikana nini kinaendelea lakini inawezekana
labda ugomvi wa wasanii hao wawili umefikia
mwisho na labda tutegemee chochote kutoka kwa
hao wasanii wawili. Kweli mbongo mpe picha story
ataandika mwenyewe
Picha hiyo inaonekana imepigwa jana, ukiangalia
vizuri kwenye hiyo picha utamwona Ne-yo kwa
nyuma, Kwahiyo iko wazi kuwa meneja wa
Diamond yupo Kenya pamoja na Alikiba. Kitu
kingine cha kutegemea ni collabo ya Diamond na
Ne-yo, Diamond alikutana na Ne-yo mwezi uliopita
Afrika kusini na aliahidi kuwa kuna kitu kinafata
kwahiyo inawezekana meneja wa Diamond yupo
Nairobi kwa ajili ya kukamilisha collabo hiyo.
Alikiba ameenda jijini humo kwa ajili ya Coke
Studio ambapo pia ataungana na wasanii wengine
wa Afrika kushirikiana na Msanii wa Marekani.
