Thursday, August 20, 2015

Gauni la Kajala lamtoa jasho ‘dizaina’ wake

KAJALA (3)Gauni la staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja, lilizua minon’gono ukumbini wakati wa Shindano la Kinondoni Talents Search (KTS) lililofanyika katika Ukumbi wa Millennium Tower, Makumbusho jijini Dar baada ya gauni hilo kuambatana na watu wa kulishika.
KAJALA (4)Staa huyo aliingia ukumbini hapo akiambata na kijana mmoja akilishika gauni lake ambapo kila alipokatiza kijana huyo alikuwa na kazi ya kuzunguka naye kuhakikisha nguo hiyo inakaa vizuri bila kujikunja kitu ambacho kiliwafanya baadhi ya watu ukumbini kuanza kulishangaa gauni hilo.
KAJALA (1)Kajala alipoulizwa sababu ya gauni hilo kushikiliwa alisema: “ Wale vijana ndiyo waliolibuni gauni langu ndiyo maana walikuwa makini kuhakikisha linakuwa sawa wakati wote,” alisema Kajala.