Wema Sepetu na Diamond
KATI ya kundi la watu wanaoongoza kwa kumwagana katika uhusiano wa mapenzi ni mastaa, lakini kwa nyakati tofauti baadhi ya mastaa waliotengana huishia kuingia kwenye uhusiano thabiti na wapenzi wengine hadi kuoana huku zilipendwa wao wakiishia kuyumba kimapenzi au kutokuwa na mpenzi wa kudumu kiasi kwamba unaweza kuitafsiri hali iyo kwa kutumia usemi wa huku sawa, kule majanga.
Wafuatao ni baadhi ya mastaa waliopitia kasumba hiyo:Katika historia ya wapendanao kwa mastaa, hawa wanaweza wakawa ndiyo kapo pekee iliyojizolea mashabiki lukuki Bongo kabla ya kumwagana kwao, lakini kwa sasa kila mtu akiwa na zake, ambapo Diamond ametulizwa na penzi la mwanamama Zarinah Hassan, ‘Zari’ na tayari uhusiano wao umejibu kwa kuzaa mtoto huku zilipendwa wake, Wema Sepetu akiwa ni majanga kwa kuwa tangu amwagane na Diamond hajatulia katika uhusiano rasmi.
Kanye West na Amber Rose
Enzi za mapenzi yao wawili hawa walitengeneza vichwa vya habari na kuwavutia watu wengi waliowafuatilia, lakini kama uhusiano mwingine mapenzi yao yaliishia ukingoni na kila mtu akachukua zake ambapo Kanye alinasa kwa Kim Kardashian na kuishia kuoana na kuzaa mtoto huku mapenzi yao yakizidi kushamiri kila siku tofauti na upande wa Amber Rose ambaye alijaribu kutulia na ‘mbishi’ Wizy Khalifa lakini mwishowe akaambulia kibuti na kubaki akitangatanga.
Janet Jackson na Jermaine Dupri
Umaarufu wa mapenzi ya wawili hawa ulikuwa gumzo nchini, Marekani kutokana na mwanadada huyo kutokea kwenye familia maarufu ya muziki iliyotambulishwa na bendi ya Jackson Five ambayo Michael Jackson alitokea huku Jermaine Dupri kwa upande wake akiwa prodyuza mkali wa muziki enzi hizo.
Baada ya kumwagana, Janet ameolewa na bilionea wa Kiarabu kutoka Qatar, Wissam Al Mana huku majanga yakiwa kwa Jermaine ambaye mpaka sasa haeleweki anatoka na nani.
Ben Affleck na J.Lo
Mapenzi kati ya diva wa muziki Jennifer Lopez na mwigizaji Ben Affleck yalikuwa yenye mvuto wa kipekee nchini Marekani, lakini kama wengine nao walimwagana kiroho mbaya huku Ben Affleck akimuoa mwanadada Jeniffer Garner na kuzaa naye watoto huku J.Lo akiwa haeleweki baada ya awali kudhaniwa atatulizwa na mkali wa muziki wa hisia, Mark Antony, lakini ilishindikana kwa mwanadada huyo kutoka na bitozi Casper Smart kabla ya kumwagana.
IYOBO NA MWENGI
Huyu ni dansa maarufu wa nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye aliwahi kutoka na mdada wa mjini, Mwengi na kuzaa naye mtoto, lakini mwishoni wakatengana kwa ugomvi baada ya Mose kuangukia kwa msanii wa muvi, Aunt Ezekiel na hatimaye kupata mtoto. Wakati huo hadi sasa Mwengi hajaweka wazi uhusiano wake jambo linaloonesha kuwa bado majanga kwa upande wake.

JACK PATRICK NA JUX
Mwanzoni walificha mapenzi yao, lakini baadaye wenyewe wakayaweka wazi mapenzi yao kabla ya kutengana baada ya Jack kuswekwa jela nchini China. Jux ameangukia kwenye penzi la diva wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee huku mambo kwa Jack ambaye bado yupo gerezani yakiwa magumu baada ya awali kutwangwa talaka akiwa gerezani na aliyekuwa mumewe, Fundikira. Hadi sasa hana mpenzi anayejulikana wazi kiasi cha kuonekana kama mkiwa.