Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omary Kopa ‘Da’ Khadija’.
Mwandishi wetu
Kutoka moyoni! Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omary Kopa ‘Da’ Khadija’ amefunguka la moyoni kwamba sasa yupo tayari kuolewa tena iwapo atatokea mwanaume mwenye vigezo anavyovihitaji.
Kwa mujibu wa Khadija, pamoja na kwamba yupo tayari kuolewa lakini hahitaji mwanaume suruali bali mchapakazi, mwenye upendo wa kweli kama alivyokuwa aliyekuwa mumewe, marehemu Jafarry Ally.
“Kuolewa ni jambo la kheri, hakuna asiyelipenda lakini mimi sipendi mwanaume asiyependa maendeleo anayependa kuoa ilimradi kaoa, napenda atakayeshirikiana na mimi kwenye kila kitu,” alisema Khadija.