Thursday, August 13, 2015

Maneno ya Diamond kuhusu collabo na Ali Kiba, Jux na Video zake MTV, Shilole na ziara ya Marekani?

Shilole amepost kwenye ukurasa wake wa @Instagram kuwa hivi karibuni atakua akifanya shoo Marekani pamoja na Mtanzania mwenzake Ommy Dimpoz. mwenyewe amesema kama yeye si muongeaji wa hilo suala anamuachia msemaji wake ambaye ndiye wakili wake aweze kulizungumzia
shhh
Jana kichupa cha Juma Jux kilionyeshwa MTV, mwenyewe amesema anashukuru na kufurahi kuona muziki wake unafika mbali, anasema anaamini itapokelewa na watu wengi zaidi na tofauti kwa wakati mmoja, pia imempa moyo zaidi wa kufanya kazi.
Anasema Video ya ‘Sisikii na ‘Nitasubiri’ alipeleka lakini hazikupata nafasi,, anajiamini kazi zake ni nzuri lakini hajui kwa nini hazijaweza kupata nafasi
juxxx
Wengi wanafahamu Diamond na Ali Kiba wana beef hawataweza kufanya collabo pamoja, leo Diamond amefunguka na kusema yeye anafanya biashara na hawezi kuacha kufanya kitu chenye manufaa kwake, amesema yupo tayari kufanya kazi na mtu yoyote na hayupo kuweka beef na mtu, anatamani kumsapoti Mtanzania mwenzake zaidi