FAIZA Ally ambaye ni mzazi mwenziye na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amefunguka kuwa mwanaye Sasha ndiyo kila kitu kiasi cha kumkatisha usingizi wake kila siku.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, alisema kutokana na mapenzi yake kwa mwanaye, kila siku anajikuta akiamka usiku mnene na kumuangalia mwanaye kwa muda mrefu kisha kumbusu na kulala tena.
“Huwa naamka usiku wa manane na kumbusu mtoto wangu na hiyo imeshanikaa, kila siku mpaka hata watu ninaoishi nao wananishangaa sana,” alisema Faiza.