Hii ni post ya Ridhiwani Kikwete kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, aliiweka hii video ya Edward Lowassa na kuandika ‘Raha ya mja kunena, kwa muungwana ni vitendo ushahidi tosha kuwa mgombea wa CCM anakubalika na ni bora kwa kazi’
Kwenye page yake ya Instagram aliweka video hiihii akaandika ‘Ni thawabu pia kutoa sifa na ni dhambi kutokubali mema yanapofanyika, hongera sana mgombea kwa kuyaona mazuri yatendekayo na mtendaji wa hayo, #Magufuli2015#MzikiwaMagufuliUtauweza?
Kwenye hii video Lowassa anasema >>> ‘Namsifu sana Dr. Magufuli kwa kazi nzuri aliyofanya, kazi nzuri sana ya barabara, nzuri sana‘