Thursday, August 13, 2015

ZITTO AFUNGUKA MAZITO SANA ASEMA ILI NCHI HII IPONE LAZIMA CCM IFE...MSIKIE MWENYEWE

Chama cha ACT kupitia kiongozi wao Zitto Kabwe kimetoa msimamo huu

"Tumekataa kuwa sehemu ya Vyama vya UKAWA kwa sababu ya MISINGI yetu ya miiko ya uongozi katika Azimio la Tabora. Hata hivyo tunajua wananchi wanataka mabadiliko ya kisiasa. Ni muhimu sana wananchi kujiona wanaweza kuondoa chama kimoja madarakani na kuweka kingine. Hivyo sisi ACTWAZALENDO tutafanya kila tuwezalo kusaidia juhudi za kuiondoa CCM madarakani. Lakini, kwa maoni yangu, hatupaswi kuwa sehemu ya Serikali yeyote itakayoundwa baada ya uchaguzi wa mwaka huu ili kuhakikisha Serikali hiyo inawajibishwa ipasavyo. Kuna haja ya kuwa na upinzani imara baada ya uchaguzi mkuu na CCM hawataweza kufanya kazi hiyo kwani wakiondoka madarakani wataifuata KANU na UNIP. Ili nchi yetu ipone lazima kwanza CCM ife." ameandika Zitto