Monday, September 28, 2015

Baada ya kufanyiwa udhalilishaji nahodha wa Azam FC, Rais wa TFF kaandika haya..

Mchezo wa soka ni mchezo ambao hupendwa na watu wengi ila kinachoshangaza wachezaji wa timu zote mbili ucheza kwa bidii kiasi kwamba inaweza tokea chuki endapo mmoja kati yao atakuwa anazidiwa mbinu na mchezaji wa timu pinzani. Kumekuwa kukifanyika matukio mengi katika soka ila kutokana na muamuzi kutokuona baadhi ya matukio hayo, Shirikisho la soka la nchi husika huchukua hatua kwa vitendo hivyo visivyo vya kiungwana kupitia kanda za video.
DSC_0035
Juma Nyoso kabla ya mechi kuanza
September 27 katika mechi kati ya Azam FC dhidi ya Mbeya City mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi, nahodha wa Mbeya City Juma Nyoso alimfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha  wa Azam FC John Bocco, licha ya kuwa muamuzi hakuona ila kupitia picha za mnato na kanda za video tukio hilo lilinaswa na kusambaa katika mitandao ya kijamii.
DSC_0111
Juma Nyoso na John Bocco
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi amethibitisha hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mchezaji aliyefanya kitendo hicho, Malinziamethibitisha hilo kupitia account yake rasmi ya twitter. Lakini hii sio mara ya kwanza kwa beki na nahodha wa Mbeya City Juma Nyoso kufanya kitendo hicho, alishawahi kumfanyia Elias Maguli na kupewa adhabu ya kufungiwa mechi nane mwanzo mwa mwaka 2015.
1