Friday, October 2, 2015

ESMA PLATNUMZ: Namshangaa Sana Diamond Kuwa na Chuki Kiasi Hicho Kwa Baba Yake Mzazi

Brighton Masalu
DADA wa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma
amemshangaa kaka yake, (Diamond) kwa
kuendeleza chuki dhidi ya baba yake mzazi,
mzee Abdul Jumaa.Akizungumza na gazeti hili
kwa njia ya simu hivi karibuni, Esma alisema
siku zote si vyema kukaa na kinyongo au chuki
dhidi ya wazazi na hata kama ikitokea ni vyema
kuyamaliza kwa mtoto kujishusha.
“Hata mimi nilishawahi kukosana na baba
yangu, lakini nilishasamehe na kusahau kabisa,
hata hapa nyumbani, ni mara nyingi tu huwa
tunatofautiana na mama lakini hata kama yeye
kakosea, huwa najishusha si kama ilivyo kwa
Nasibu (Diamond) kuwa na chuki kali kiasi
hicho dhidi ya baba yake, ” alisema Esma.
Source:GPL