Mayasa Mariwata
MASTAA wa filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ pamoja na Skyner Ally ‘Skaina’ wanadaiwa kufanya uchafu baada ya picha za wawili hao wakionesha mahaba hadharani kusambaa.
Chanzo kinaanika kuwa wawili hao hivi karibuni walikutana katika Ukumbi wa KD, Kijitonyama ambapo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa kwa Rayuu huku wakionesha mahaba ya mtu na mpenzi wake ndipo picha hizo zilipopatikana.
Baada ya madai haya, Amani lilimvutia waya Skaina ambapo simu yake haikuwepo hewani lakini lilipomtafuta Rayuu alisema kuwa haoni kama kuna cha ajabu.
“Sina tabia chafu, yale yalikuwa ni mambo ya Kizungu tu maana ilikuwa bethidei na mwenyewe (Skaina) katika kipindi cha kulishana keki aliamua kutumia mdomo,” alisema Rayuu.