Friday, November 20, 2015

Kijana Afariki Dunia Baada ya Kufanya Mapenzi na Nguruwe Wilayani Ludewa

Kijana mmoja aitwaye Simon Dustan Mwanjavala maarufu kama Mwachakala (15) mkazi wa kijiji cha Mbwila kata ya Luana wilaya ya Ludewa mkoani Njombe amefariki dunia muda mchache baada ya kukutwa akifanya mapenzi na Nguruwe

Tukio hilo la kustaajabisha limetokea jana wilayani Ludewa baada ya kijana huyo "kufumaniwa" akifanya mapenzi na mnyama huyo, ndipo walipomkamata na kumfunga kamba mikono yake na miguu ili asikimbie
Baada ya majirani kumuona kijana huyo akimbaka nguruwe huyo kwenye banda la mnyama huyo walikwenda kumwambia baba yake mdogo ambao kwa pamoja walimkamata kijana huyo, ambaye alikiri kufanya kosa hilo
Alipoulizwa sababu zilizomfanya kufanya mapenzi na nguruwe, alisema alikuwa na hamu ya kufanya tendo hilo
Kutokana na kitendo hicho waliamua kumvua nguo zote na kumfunga kamba na kumpa kichapo  kisha wakamuacha kwa muda kwenye eneo la tukio, na walipokuja kumfungua kamba na mwenyekiti wa kijiji hicho, alidondoka na kufariki dunia papo hapo