DUNIANI kuna mambo! Wakati saluni za masaji (massage therapy) zikiendelea kuanzishwa kila kukicha katika Jiji la Dar kwa lengo la kutoa huduma ya kitabibu, ‘kama kawa’, kile kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers kimevumbua mazito, twende pamoja.
Ni Jumanne iliyopita, majira ya mchana wa jua kali, OFM kwa kushirikiana na polisi walimnasa mhudumu mmoja wa kike kwenye masaji iliyoko maeneo ya Sinza Mori, Dar akiichakaza amri ya sita na mteja wake.
ENEO LA TUKIO
Wawili hao walinaswa wakifanya dhambi hiyo ya kudhamiria ndani ya chumba kimoja cha kutolea huduma katika jengo lenye masaji hiyo. Wote walinaswa wakiwa hawana nguo hata moja!
ILIKUAJE?
Siku moja kabla ya siku ya tukio, msomaji wetu mmoja alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global Publishers na kumwaga maneno haya:
“Nyie watu wa Global, nimewahi kusoma kwenye magazeti yenu mkiwa mmetoa hizi saluni zenye masaji ndani. Ninavyojua mimi kazi ya masaji ni kama kutoa huduma za kitabibu kwa kukanda wateja ili kuimarisha mishipa ya miili yao na husaidia kuondoa uchovu.”
Chumba cha habari: “Haswaa! Lete habari!”
Chanzo: “Sasa mbona hapa Sinza Mori, maeneo ya Meeda kuna saluni ya masaji, yenyewe inatoa mpaka huduma ya ngono kwa wateja wake wa kiume! Hivi hapa ninapozungumza na wewe si ajabu kuna huduma hiyo inaendelea.”
MTEJA HUSHAWISHIWA
“Tatizo la hapa ni kwamba, mteja wa kiume akifika atashawishiwa na mhudumu kwa namna yoyote ile ili afanye naye mapenzi kwa sababu akifanya hivyo ndiyo anajiongezea kipato.
“Sasa basi mtashangaa kuona ndani ya mikoba ya watoa huduma kuna kondomu na ukizunguka kwenye jalala la taka utaziona zilizotumika. Hebu liangalieni hili.”
OFM YAJIFANYA MTEJA
Mara baada ya kupata taarifa hizo, OFM ilisimama mguu sawa na kuanza safari. Kamanda mmoja wa OFM alijifanya mteja na kutimba kwenye saluni hiyo na kuulizia huduma ya masaji, pia akagusia suala la huduma ya ngono ambapo mmoja wa wahudumu hao alikubali na kumtaka asiwe na wasiwasi.
MTEGO WAUNDWA
Baada ya kuona mambo yapo kama madai yalivyosema, ndipo kamanda aliaga akizuga angerudi baada ya kutoa pesa mtandaoni. Akaenda kutoa taarifa kwa makamanda wengine wa OFM ambao waliweka mtego wa saa 24 nje ya saluni hiyo.
Novemba 10, mwaka huu, saa 6 mchana makamanda hao waliliona gari aina ya Toyota Harrier ikiendeshwa na mwanaume, iliingia ndani ya saluni hiyo.
Ndipo OFM walipotoa taarifa kwa vyombo vya usalama (polisi) na kuweka mtego kwa mmoja wa makamanda hao kuingia upande mwingine wa saluni ambapo kuna huduma ya kunyoa lengo ni kuona nini kinaendelea ndani.
OFM NDANI YA TUKIO
Baada ya kupita robo saa tangu mwanaume yule aingie, ndipo OFM wakiwa na polisi walizama kwenye saluni hiyo na kuwahoji wahudumu waliokuwepo sehemu ya kupokelea kuhusu chumba alichoingia mwanaume yule lakini kabla hawajafika mbali, zilisikika sauti za mahaba kutoka kwenye chumba kimoja.
Polisi na OFM walishika mlango ambao haukufungwa kwa ndani na kuzama ndani ya chumba hicho na kumkuta mrembo aliyedai ni mhudumu na yule mwanaume wa Harrier wakiwa kama walivyozaliwa.
UTETEZI WA MHUDUMU
Katika utetezi wake, mhudumu huyo alisema mwanaume huyo ndiye aliyemshawishi kukutana kimwili baada ya kutaka aina ya masaji inayoitwa ‘body to body’ ambayo katika maelezo yake, kitendo hicho hufanyika bila nguo yoyote kati ya mteja na mhudumu.Hata hivyo, utetezi wake ulipingwa vikali na mteja wake aliyedai alifika katika saluni hiyo kwa ajili ya ngono kwa vile mara kadhaa hufika kupatiwa huduma hiyo huku akiwaonesha OFM kondomu aliyokuwa nayo mhudumu huyo.
Mhudumu huyo na mteja wake walichukuliwa na vyombo vya dola kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria.
Credit: GPL