Tuesday, November 10, 2015

Mtaalam wa IT Hospitali ya Regency auawa kikatili

REGENCY MTAALAM WA IT (9)
Maximillian Katikiro, enzi za uhai wake .
Na Makongoro Oging’na Haruni Sanchawa
DUNIA mbaya! Ni tukio lililowashangaza wafanyakazi wa hospitali kubwa ya binafsi nchini, Regency iliyopo jijini Dar pale walipopata taarifa za kuuawa kwa Mkuu wa Kitengo cha Information Technology (IT), Maximillian Katikiro (35) usiku wa kuamkia Novemba 2, mwaka huu.
REGENCY MTAALAM WA IT (8)Shughuli za maziko kwa marehemu.
Uwazi baada ya kupata taarifa za msomi huyo kuuawa lilifika nyumbani kwa wazazi wake, Gongo la Mboto, Dar na kukutana na baba mzazi wa marehemu.
Katika mahojiono kuhusiana na kifo cha mwanaye, mzee Katikiro alisema siku ya tukio, kijana huyo akiwa kwake Kitunda alimuaga mkewe anakwenda Yombo kukutana na mtu kwa mazungumzo ya biashara.
Alisema marehemu alichelewa kurudi hivyo ilifika wakati mkewe akaanza kumtafuta kwenye simu lakini akawa hapatikani.
REGENCY MTAALAM WA IT (7)…Waombolezaji.
Usiku sana, mke wa marehemu alitoa taarifa kwa wakwe zake, pia alimpigia simu rafiki yake mmoja na kumtaarifu kuwa, mume wake hajarudi na simu yake haipatikani kitu ambacho si kawaida yake.
“Yule rafiki wa mke wa Maximillian alikwenda nyumbani kwa marehemu Kitunda, wakaungana na kuanza  kutafuta vituo vyote vya polisi na meneo mengine. Kilichosikitisha ni kwamba, walifika sehemu wakakuta mwili wa Maximilian umetupwa maeneo ya Mwanagati,  hatua kadhaa kutoka nyumbani kwa marehemu.
REGENCY MTAALAM WA IT (5)“Mimi nilipokea simu kutoka kwa watu waliokuwa wakimtafuta baada ya kufanya mawasiliano na Polisi wa Kituo cha Stakishari,” alisema mzee huyo.
Akaendelea: “Nilihakikishiwa kuwa ni mwanangu, wakaniuliza wanafanyaje jibu nililowapa ni kuwa msiba uletwe hapa nyumbani Gongo la Mboto kwa maana ya kuanza taratibu nyingine pamoja na uchunguzi kisha maziko.”
REGENCY MTAALAM WA IT (4)Akizidi kuongea kwa masikitiko, mzee Katikiro alisema kuwa tangu utoto wake, kijana wake hakuwa na ugomvi na mtu na hakuwahi kusikia malalamiko kutoka kwa watu hivyo haelewi kilichompata mwanaye.
Hata hivyo, taarifa zilizonaswa na gazeti hili zinaonesha kuwa, siku ya tukio marehemu alikodi bodaboda sehemu kwenda nyumbani kwake, Kitunda kwa mapatano ya malipo ya shilingi 2,500.
Inadaiwa kuwa,  walipokaribia marehemu alimwambia dereva amefika akamlipa shilingi 2,000 hivyo marehemu alipungukiwa  shilingi mia tano jambo ambalo bodaboda  hakukubaliana nalo.
REGENCY MTAALAM WA IT (1)Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye kaburi.
Taarifa hizo zinasema kuwa kwa kupishana lugha, marehemu alimwambia dereva amrudishe alikomtoa jambo ambalo dereva alikubaliana nalo.
“Alipomfikisha kule, dereva aliwaambia wenzake kuwa, abiria huyo amemzingua, hataki kumlipa pesa yake.
“Nasikia wenzake walianza kumshambulia marehemu mpaka kumuua kisha kwenda  kuutupa mwili eneo la Mwanagati,” kilisema chanzo kimoja.
Marehemu Maximillian alizikwa wiki iliyopita katika Makaburi ya Air Wing, Ilala jijini Dar es Salaam.