…Akiomba asamehewe.
Jambo limezua jambo! Habari ikufikie kwamba Wizara ya Elimu nchini inamshughulikia yule Ticha Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyopo Upanga jijini Dar (jina tunalo) ambaye hivi karibuni alinaswa akiwa ofisini kwake na mke wa mtu ambaye ni mzazi wa mwanafunzi wake.
Mwalimu Mkuu huyo alivyonaswa siku ya tukio.
Mwalimu huyo alinaswa ofisini kwake na mzazi huyo huku walichokuwa wakitaka kufanya ikiwa ni siri yao.
Kwa mujibu wa habari hiyo, mzazi wa mwanafunzi huyo alimwambia mwandishi wetu kuwa mwalimu huyo alimpigia simu na kumwita aende shuleni hapo wakaongee lakini hakwenda kwa kuhofia usalama wake.
Siku ya tukio hilo waandishi wa habari walifika shuleni hapo na kukuta kuna kikundi kidogo cha watu na walipojipenyeza ndani walimkuta mwalimu mkuu huyo akiwa katika harakari za kufunga zipu.
Pamoja na fedheha hiyo, mapema wiki hii wanahabari wetu walifika shuleni hapo na kumkuta mkuu huyo wa shule akiendelea kuchapa mzigo kama kawaida ndipo wakatinga wizarani kujua kama kuna hatua zozote zilikuwa zimechukuliwa dhidi yake.
Hata hivyo, waandishi wetu walipofika wizarani walielezwa kwamba tayari maelekezo ya namna ya kumshughulikia mwalimu huyo yalikuwa yametolewa kwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Kielimu wa Ilala aliyetajwa kwa jina moja la Mapunda.
Tulipofika kwa afisa huyo wa elimu alisema kuwa kosa hilo ni kubwa hivyo ni lazima mwalimu huyo achukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kutimuliwa kazi kwa mujibu wa maelekezo ya Wizara ya Elimu.
“Tumeagizwa kufanya uchunguzi, ikibainika kweli ametenda kosa hilo lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake,” alisema Mapunda.
Katika tukio hilo, mwalimu huyo alipigwa pingu na polisi ambapo alipelekwa kwenye kituo cha polisi kilicho karibu na eneo hilo hilo kabla ya kuachiwa baada ya kuchukuliwa maelezo.
credit:GPL