Mwanamuziki
Rehema Charamila ‘Ray C’ amekumbwa na aibu ya aina yake baada ya hivi
karibuni kuvuja ‘video’ inayomuonesha akiwa mtupu huku akikata viuno.
Video hiyo ambayo haimuoneshi uso lakini
mkono wake wenye tatuu unaonekana ilivuja kupitia ukurasa wake wa
Instagram, jambo ambalo liliwafanya watu washangae.
Katika video hiyo anaonekana kama Ray C
yuko faragha na ‘mtu’ wake na wakati watu wakiendelea kuijadili,
ilitolewa fasta kwenye ukurasa wake.
Hata hivyo, wakati ikitolewa, tayari wajanja walikuwa wameshainasa hivyo kusambaa kama moto wa kifuu.
Akizungumza kuhusiana
na video hiyo, Ray C alikiri kuwa ni yake, ilikuwa kwenye simu yake
lakini aliibiwa na aliyemfanyia uhuni huo ni aliyemuibia.
“Ni kweli ni yangu ila siyo mimi
niliyeiweka kwenye ukurasa wangu wa Instagram. Hiyo video ilikuwa kwenye
simu yangu sasa imeibiwa na mtu aliyeiba ndiye aliyenifanyia kitu hicho
kibaya, hapa najipanga kwenda polisi,” alisema Ray C.