JIJI LETU

Tuesday, December 1, 2015

TAARIFA MPYA YA KESI YA KAFULILA :::MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA WAKILI WA HUSNA DHIDI YA KAFULILA.

Jana Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini ilofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka kwa wakili wa Husna Mwilima kutaka Mahakama Kuu isiendelee na kesi hiyo kwakuwa Mhe Kafulila hakufuata taratibu katika ufunguzi wa kesi hiyo.

Katika utetezi wa wakili wa Kafulila Daniel Lumenyera, Tundu Lissu waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo la wakili maarufu Fungamtama kwa hoja kuwa ni usumbufu kwa mteja wao na halina mana yoyote kwa kesi ya Msingi.


Leo Jaji anaesikiliza kesi hiyo Bi Leila amezingatia ombi la Fungamtama na utetezi Lumenyela na kuamua kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa Husna na kumtaka Husna Mwilima kumlipa Kafulila gharama za usumbufu kwa kuweka mapingamizi yenye sura ya kupoteza muda na usumbufu.

leo Mahakama imendelea na hoja ya kutathimini gharama ya dhamana ambayo Mhe Kafulila atapaswa kuweka kama dhamana ya kesi ili kesi ya msingi iweze kuanza.

Uamuzi kuhusu kiasi gani Mhe Kafulila atalipwa kama dhamana utatolewa kesho na Mahakama.
at 10:40:00 PM
Newer Post Older Post Home

categories

AFYA AJALI AJIRA BIG BROTHER BONGO MOVIE Bongofleva Bongomovie BUNGENI ELIMU FASHION FIESTA FUMANIZI Habari Za Mitaani HIP HOP Instagram KIMATAIFA KITAIFA MAAJABU Madawa ya kulevya MAGAZETI MAPENZI MBELE MICHEZO RECORD SIASA TECHNOLOGY UDAKU UKATILI UTAFITI VITUKO WASANII WhatsApp Videos

Popular Posts

  • Kumekucha: Mwinyi, Mkapa, Aman Abeid Karume Wakutana Rasmi Kuwajadili Wagombea Urais Wa CCM
  • UTABIRI ''KUNA MGOMBEA URAIS ATAKAYEKUFA AKITAFUTA URAIS JUKWAANI>>SOMA HAPA KUJUA UKWELI
  • Magazeti ya Tanzania December 2 2015
  • Vigogo TRA Wakutwa na Mamilioni Nyumbani Kwao
  • HUYU SALAMA WA MKASI HAISHI VITUKO, TAZAMA HIZI PICHA NNE DAH NI SHIDAA
  • JAMANI KUMBE BIASHA YA U SOCIALITE INA LIPA>>HEBU JIONEE NDINGA YA MASOGANGE ANAYOENDESHA>>>>LEVEL ZA ZARI>>>>>PICHAZ
  • JEURI YA PESA! WEMA ATANGAZA DAU LA MILIONI ATAKAYEMUONA MBWA WAKE ALIEPOTEA
  • HII INAHUSIKA, OBAMA AMPA SHAVU MSANII HUYU WA BONGO...JIONEE HAPA
  • Kampuni Ya UDA Yaikana Familia Ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
  • JK ATEMBELEA MAJERUHI MKUTANO WA KAMPENI WA DK. MAGUFULI MORO.
Awesome Inc. theme. Powered by Blogger.