HOTELI ya kimataifa ya Serena jana ilikumbwa na
msukosuko wa kuandamwa na waandishi wa habari
baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa imefungwa
kwa amri ya serikali kwa kosa la kukwepa kulipa
kodi.
Tetesi hizo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya
kijamii jana asubuhi, zikieleza kuwa maofisa wa
Mamlaka ya Mapato (TRA) wameifunga hoteli
kufunga kwa kukwepa kuliko kodi serikalini.
Mbali ya kusambazwa kwa uvumi huo, zilitumwa pia
picha zilizokuwa zikionyesha sehemu ya hoteli hiyo
ikiwa imezungushwa uzio uliokuwa na rangi nyeupe
na nyekundu ambao ni alama inayotumika
kuonyesha kusitisha kwa huduma katika eneo hilo.
Tetesi hizo zilikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa
uongozi wa hoteli hiyo ulikuwa mbioni kubadilisha
jina kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.
Hata hivyo, mwandishi wetu baada ya kufika
hotelini hapo kwa lengo la kufuatilia ukweli wa
tetesi hizo alikuta shughuli za ukarabati wa sehemu
ya kupokea wageni zikiendelea, huku wageni
wakielekezwa kutumia mlango wa dharura ambako
kumetengezwa sehemu ya muda ya kupokelea
wageni.
Uongozi wa Hoteli ya Serena kupitia Mkurugenzi wa
Mauzo na Masoko, Seraphine Lusala, ulilazimika
kutoa taarifa kwa vyombo vya habari ukikanusha
kufungwa kwa hoteli hiyo na kusisitiza kuwa
kinachoendelea hotelini hapo ni matengenezo.
“Si kweli kama hoteli imefungwa, tunafanya
matengenezo na yalikuwa yafanyike tangu miaka
mitatu iliyopita, kilichofanyika sasa ni kubadilisha
eneo la mapokezi yaliyohamishiwa milango mingine
na tumeanza na eneo hilo pamoja na sehemu ya
mazoezi,” alisema Lusala.
Alisema matengenezo hayo yanalenga kuifanya
hoteli hiyo kuwa ya kiwango cha juu zaidi na
yatachukua miezi 10.
Lusala alisema awamu ya kwanza ya matengenezo
itachukua miezi minne na miezi minne ijayo itahusu
matengenezo sehemu ya vinywaji, chakula, eneo la
uwanja na baadaye maeneo mengine ya wazi.