Monday, January 11, 2016

Zari ampeleka Tiffah kufanyiwa tambiko

3
Stori:Musa Mateja, 

DAR ES SALAAM: Utamaduni! Mzazi mwenzake staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’, anadaiwa kumpeleka mwanaye Latiffah Nasibu ‘Tiffah’ (miezi 5) kijijini kwao Uganda ambako amefanyiwa tambiko la kimila huku Diamond akiichomolea mbali safari hiyo, Ijumaa Wikienda lina kitu cha kushika mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo linalofanywa na makabila mengi ya Afrika, lilijiri Ijumaa iliyopita mjini Jinja, nchini humo na kuhudhuriwa na wana ukoo wa Zari, wakiwemo pia wajomba huku bibi Zari akiwa ndiye mwenye shughuli hiyo kwa kusaidiwa na mwanaye, bibi Tiffah ambaye pia ni mama mzazi wa Zari, Halima Hassan.
ZARI ALITOKEA BONGO
Chanzo chetu kimesema kuwa, Zari aliondoka jijini Dar es Salaam siku moja baada ya kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya ambapo alifunga mizigo yake kuelekea nyumbani kwake Afrika Kusini kuwachukua wanaye wengine, Pinto, Didy na Quincy Ivan Ssemwanga na kuambatana nao hadi Jinja kwa bibi yake.
TWENDE NA CHANZO
“Ebwana ngoja nikupe habari ya kushangaza juu ya huyu mzazi mwenzake na Diamond, Zari. Sikuwahi kutegemea kama mwanamke huyu ninavyomuona na mambo yake ya Kizungu-zungu lakini kafunga safari hadi kwa bibi yake, Uganda kwa ajili ya kufanya mambo ya kimila kwa mtoto wake, Tiffah. Safi sana. Nasikia hata wale wengine walifanyiwa walipokuwa watoto kama Tiffah.
1“Juzikati tu, baada ya kula Mwaka Mpya alimuomba Diamond waende wote Uganda kwa ajili ya kumfanyia tambiko Tiffah, lakini Diamond alichomoa safari hiyo, hakwenda.
“Nilizungumza na Diamond juu ya suala hilo akasema kuwa, yeye ameshindwa kwenda kutokana na kutoamini sana mambo hayo ya mila na desturi ambazo si za kabila lake,” kilisema chanzo hicho.
MBUZI ACHINJWA
Chanzo kiliendelea kuweka wazi kwamba, miongoni mwa mambo yaliyofanyika kwenye shughuli hiyo ni kuchinjwa kwa mbuzi aliyekomaa ambapo nyama yake ilipikwa mpaka kuiva bila kuungwa na vikorombwezo vyovyote kisha watu wakala.
ZARI APIKISHWA KIENYEJI
Katika hali ambayo mashabiki wake hawakuizoea, Zari katika mwendelezo wa mila hiyo, alielekezwa kupika nyama ya mbuzi huyo kwenye sufuria kubwa lililofunikwa juu kwa majani ya migomba ya ndizi badala ya mfuniko. Pia, Zari alitumia jiko la kuni lenye mafiga matatu kupika huku likitoa moshi.
zarinaaaaKWENYE MSOSI
Baada ya msosi huo kukamilika, Zari, watoto wake, wajomba zake, mama yake na ndugu wengine walikaa kwenye mkeka nje na kula kwa pamoja. Inadaiwa baada ya mlo ndipo wazee wenye kuaminiwa katika jamii walisema maneno yenye heri kwa ajili ya makuzi ya Tiffah.
DIAMOND ILIKUWA ATAMBULISHWE RASMI
Habari zaidi zinasema kuwa, licha ya Tiffah kufanyiwa ‘madongoloji’, kama Diamond angekubali kwenda ilikuwa akatambulishwe rasmi ukweni kwake ambapo ndugu wa Zari wangeonana naye ‘laivu’ na kumkaribisha kama mchumba wa Zari.
DIAMOND ATOA NENO KWA WIKIENDA
Baada ya kupewa mchongo huo, Wikienda lilimtafuta Diamond ana kwa ana kwa nia ya kutaka kujua kwa nini aligoma kuambatana na Zari nchini Uganda ili kufanikisha tambiko la mwanaye ambapo alisema hajagoma kwenda bali majukumu yaliyo mbele yake yalimzuia.
11850013_466174470220105_1281926624_n“Mimi sijagoma kwenda Uganda na Zari kama wengi wanavyoweza kusema, ila ukweli ni kwamba nashughulikia studio na ofisi yangu mpya. Si unajua tumehama pale tulipokuwa (Sinza-Mapambano) na sasa tupo hapa (Sinza-Mori).
“Nisipokuwepo kwenye ufungaji huu wa vyombo na samani hizi hakuna anayeweza kujua mimi nataka ofisi hii iweje na studio ifungweje. Kama ningekwenda basi yote yangefanyika,’ alisema Diamond.