Friday, February 19, 2016

Baraka Da Prince azungumzia kauli ya Ray Kigosi na maji.

barakaa
Staa wa bongo fleva Baraka ameongelea issue ya Ray ya kunywa maji na kuwa mweupe nakusema kuwa kitu hicho ni mara ya kwanza kukisikia maishani mwake, kwani hajawahi kusikia popote duniani.
Ameanza kwa kucheka…..”hahahahahaaa, mi ndo mara yangu ya kwanza kusikia hiyo, sijawahi kusikia popote duniani, ila labda ni kweli (huu anacheka) ila mi sijui kama maji yanabadilisha rangi“, alisema Baraka da Prince ambaye ni mweusi.
Baraka aliendelea kusema kwamba yeye haamini kabisa katika hilo na napenda rangi yake na hafikirii kubadilisha muonekano wake, kwani hivyo alivyo mashabiki wanampenda, licha ya Ray kusema pia anafanya hivyo ili awe na muonekano mzuri kwa jamii.
Siamini hayo mambo, na napenda rangi yangu jinsi ilivyo, sasa kwa nini nibadlishe, siamini kama watu wanapenda rangi nyeupe, mi sina rangi lakini napendwa, naperform mpaka watu wanalia, mpaka napewa tuzo, kazi nzuri ndio inafanya mashabiki wapende kazi yako na wakukubali, mbona mi bonge la HB (akimaanisha handsome boy) na weusi wangu na watu weupe nawakalisha, mi handsome“, alisema Baraka da Prince.
Akijibu post ya Godzila akimtaka Baraka da Prince akatumbukie baharini ili awe mweupe, amesema yeye na Godzila wanataniana, hivyo hana tatizo na hilo kwani pia anamchukulia kama kaka yake, hivyo haijamsumbua.