Msanii wa muvi Tanzania Vincent Kigosi maarufu kama Ray ameweka wazi kuwa hatumii mkorogo kama Nay wa Mitego alivyomtuhumu kwenye wimbo wa shika adabu yako badala yake hunywa maji mengi na kufanya mazoezi kitu kinachomfanya anakuwa mweupe.
Lakini jibu la Ray limepokelewa kwa njia ya kuchekesha zaidi baada ya watu mbalimbali ikiwemo mastaa kupost picha instagram na kuandika kuwa watafuata ushauri wa mwigizaji huyo kwa njia ya kumdhihaki ambapo sasa imekuwa kama kiki kupitia mtandao huo.
Kwa upande wake baba kijacho aliyepoteza ndoto zake,Idriss Sultan alipost video inayomwonyesha akijaribu kujipaka mkorogo na baadaye kukumbuka ushauri wa Ray na kuanza kufakamia maji na kufanya mazoezi.![ray 2](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_udvEcAcmq4ZOmmtMurbobQdiMP8OousA23sDGVfMNEsPiuvq_bvuvQjckQWKmTySp1LE1HvC4u9RIiGxk59m4rJDumMFFDstKDklVYCHpdydKn_rUxpDdtS80xoSdaLCSwAmbFF0ulDtNeABGf-lyiFWxYFg=s0-d)
Kwa Godzilla ndio ilikuwa balaa alipost picha zikionyesha watoto weusii na kuandika #Simtanki kumaanisha watoto hao wanahitaji tanki,na nyingine ambayo amepost watoto weusi wakijirusha baharini na kumtaka Baraka da prince naye afanye hivyo.![ray4](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s4gjo5RzKst5SLFPsFMGZeo8eIzT1nApBEn4Jk7yIlPOlrUKFb2iav7SH3RJRvlcougzutErAZRXUj64SzTZAdJqf_QkvMgl2cziEw2Gc6DcQAf4b7qeEAYhNQ-vx9v_oG3PR6l5vgnN9lZh61s-V4ZdWN=s0-d)
![ray5](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s8CY3Z2c9jGr3gAWzD_ksN84pdkVqTZojPIk0qrIIB2Tx0xGeq1ANYWz9xGOxtE8h8AWUGbD6UBmJ3JiamdWz1mcae_eYkqu_26AJEqGdTLGyJ9NVB9badywViM6dKl3I7w6wkQioB7F81haQX9SOFYNZ3=s0-d)
![ray6](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_v9u_uZpcnt-hML44sSswBahL6pwoajTtVVLjHTUxEwsAIszjjuWBp1159iJGTOxnBMZg40CoLU3RpMx8RF-wQDr8fe3-v0BFMNy0TkyD9qrh2GKpQXPHHth3qzVaza3HyrUOdyzzmUHrp21z7R5oOo-nA=s0-d)
Kwa upande wake Kitale amepost picha ya watoto weusi tii inayosomeka Kaka Ray tunaomba mma,ambapo picha hiyo ilipostiwa pia na msanii JB na wengineo.![ray1](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sdlLOgEY4g9bB5aGtYZfWQDPRLIXOhRaaqg8xuwrPFQMdXQ9S7FnBQhGTyX1a0H9LC8OmxWUePVQqSKOQtjiuVL-NxsbWQhxr6q6Ovn61HqD9OZ-1zAH97poeeBvT_9vl-RoqXU8j-RXRctEyh2G1919Q=s0-d)
Hao ni baadhi ya mastaa waliojitokeza kumdhihaki Ray kwa jibu lake hilo.