Tuesday, March 22, 2016
Baba yake Peter Manyika wa Simba Adai Mwanane Ameshuka Kiwango Kutokana na Kuendekeza Mapenzi
Baada ya kuona kipaji cha mwanae kikipotea wakati akiwa na kazi kubwa ya kulitumikia taifa lake, Baba mzazi wa kipa wa klabu ya Simba, Peter Manyika Jr, Manyika Peter ameibuka na kumkoromea mwanae.
Baba mzazi huyo alisema kinachomponza mwanae ni kukosa nidhamu na pia kutekwa na mahusiano ya kimapenzi aliyonayo kwa sasa.
Akizungumza kwa uchungu, nyota huyo wa zamani wa Sigara, Mtibwa Sugar, Yanga na Taifa Stars, alisema mwanaye anapotea kwa sababu ya kuendekeza starehe na huwa anajisikia vibaya anaposikia akiwajibu mbovu waanahabari na hata viongozi wake kuhusiana na sakata lake la mambo ya mapenzi.
“Amesajiliwa Simba afanye kazi siyo kula mshahara wa bure na kuishia kukaa benchi, viongozi hawana tatizo kama angekuwa msaada angepangwa lakini yeye ajiulize na hayo mahusiano aliyonayo kama yanamsaidia katika kazi yake?” Alihoji bila kumuweka hadharani binti huyo anayemzingua Manyika
“Akipata jibu na atarudi kwenye mstari, kama mzazi najisikia uchungu sana kwa yale anayoyafanya mtoto wangu kwa sababu najua maisha ni nini lakini yeye anaona mjanja ila nina shaka hapo mbele asije akaumizwa vibaya,” alisema Mzee Manyika.
Aliongeza, “Nimecheza nafasi kama yake kwa mafanikio makubwa, ndiyo maana nasema kwa uchungu kwamba jibu ni mwanangu wala siyo viongozi yeye ndiye chanzo kwa sababu wasingeweza kutupa pesa yao bure kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu kama pambo bali kwa ajili ya kufanya kazi yao,”
Pia alisema kuwa hawezi kumkataza mwanae kuendelea na mapenzi na mwanamke aliyenaye, isipokuwa ni vema kuangalia mustakabali wake kwa sababu mtaji wake ni kipaji cha soka na akizembea atakuja kujuta mbeleni.
“Kipindi nilichokuwa nacheza na staa katika jamii nilifuatwa na wanawake wa kila aina na wengine kutaka wagharamikie kwa kila hali lakini nilikuwa na msimamo na kupuuza mambo yao na sitaki mwanangu aangamie,” alisema Manyika.
Kipa Manyika aliposakwa kwa njia ya simu, hakupokea simu aliyopigiwa, lakini kocha wa makipa wa Simba Adam Abdallah, alisema kinachofanya Manyika Jr, asugue benchi ni kutokana na kukosa nafasi mbele ya Vincent Angban aliyepo juu kwa sasa lakini mchezaji huyo si mbaya