Nyota wa filamu Nchini Burundi na Rwanda Ibrahim Ismael ‘Ic’u Ibrah’ amefunguka kwa kusema kuwa moja kati ya ndoto zake ni kuigiza filamu moja kubwa na Madame Wema Sepetu kwani ni msanii anayeamini kuwa ni mwigizaji mzuri na anaweza kuigiza.
“Nashukru kwa mara ya kwanza kuigiza na actress kutoka Tanzania Shamsa Ford, lakini nitafurahi sana nitakapofanikiwa kuigiza na Wema Sepetu kwa gharama yoyote, anajua sana mimi ni kama Kanumba vile,”anasema Ibrah.
Msanii huyo nyota raia wa Burundi amedai kuwa anazikubali sana kazi za marehemu Steven Kanumba huku akiamini kuwa msanii huyo alikuwa bora kwa Tanzania anatamani awe kama Kanumba katika uigizaji na hilo anaamini kuwa atalifanya.
Ibrah ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini Burundi na tayari amefanikiwa kutayarishaji na kuigiza filamu kali na za kusisimua kama vile Wife of my Life, Fake deal, Seconde na Questions House ambazo zimeteka soko la filamu Burundi, Rwanda, Congo DRC na sehemu nyingine.