Thursday, March 31, 2016

Nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa Ulaya Zatangaza kusitisha Ufadhili wao Kwa Bajeti ya Serikali ya Tanzania Kisa Uchaguzi wa Zanzibar


Nchi 10 kati ya 14  za umoja wa Ulaya zimetangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.

Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali yamarekani (MCC) kuondoa msaada wa dola 472 ( Trilioni 1 )  wa kufadhili miradi ya maendeleo wakidai kuwa uchaguzi wa Marudio zanzibar haukuwa huru na wa haki.

Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada toka mataifa ya nje katika bajeti ya mwaka 2015/2016. 

Chanzo: BBC