Monday, April 4, 2016

Jide: Sijampiga Kijembe Gardner G Habash Kwenye Wimbo Wangu Mpya...

MKONGWE wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide, amefunguka kuwa katika wimbo wake mpya wa Ndindindi, hajampiga kijembe  aliyekuwa mumewe, Mtangazaji Gardner G. Habash kama wengi wanavyodhani.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Jide alisema wimbo huo ulitungwa na watu wake tofauti na yeye kuukamilisha hivyo kwa kuwa umebeba ujumbe mzito ni rahisi mtu kuhisi amemuimba mtu fulani kumbe yeye aliimba kwa ajili ya mashabiki wake wote.


“Sijampiga kijembe huyo wanayemsema (Gardner). Mimi nimetumia utunzi wangu kuwakilisha yale yanayotokea katika jamii mbalimbali sasa kama mtu anaona umemgusa fulani atakuwa amejiongeza tu lakini mimi sikumaanisha mtu mmoja bali  ujumbe kwa mashabiki wangu wote,” alisema Jide.

Kwenye wimbo huo kuna sehemu Jide kaimba; “Niliwezaje kutoa vyote ili hali wewe ulininyima vyote” ambapo iliaminika amemzungumzia Gardner.