Wednesday, April 6, 2016

Msururu Wa Wapenzi Kwa Mastaa Hawa, Ni Fasheni?

12479390_1264053230275845_15732377_nNASIBU ABDUL ‘DIAMOND’
Na Gladness Mallya
INGAWA kuwa na msururu wa wapenzi ni hulka ya mtu binafsi, lakini katika maisha ya kawaida, inadhaniwa kuwa mastaa wengi wametumia umaarufu wa majina yao kama moja ya njia za kuwafanya wawe na idadi kubwa ya wapenzi.
Na hii siyo Ulaya na Marekani pekee, bali kote barani Afrika, Tanzania ikiwemo. Katika mkumbo huu, tunawakuta watu kama Katie Price ‘Jordan’, Kim Kardashian, Jennifer Lopez ‘JLO’, Charlie Sheen au Jude Law kwa kule mamtoni, wakati katika bara letu, marehemu Fella Anikulapo Kuti ndiye kinara.
Hili jambo halikuanza leo, ingawa katika miaka ya karibuni vitendo hivi vimekuwa vikifanyika wazi wazi na kuonekana kama fasheni tofauti na kipindi hicho ambacho watu maarufu waliingia katika uhusiano na watu wengi lakini kwa siri kubwa.
maxresdefault
EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’
Wafuatao ni baadhi ya mastaa wa fani mbalimbali wa hapa nyumbani, ambao wanafahamika kwa kuwa na idadi kubwa ya wenza waliowahi kushirikiana nao kimapenzi.
Ni staa anayefanya vizuri kwa sasa kwenye ulimwengu wa Muziki wa Kizazi Kipya, lakini historia yake ya kimapenzi inamuonesha kama mmoja wa wasanii waliowapitia mabinti wengi.
Tangu alipopata umaarufu, Diamond ameripotiwa kutoka kimapenzi kwa nyakati tofauti na Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jacqueline Wolper kuwataja kwa uchache kabla ya kuja kutulia mikononi mwa Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.
Naye ni staa mwingine mkali katika Bongo Fleva, anayeonekana kuwa kiwembe kwani kwa nyakati tofauti aliwahi kutoka kimapenzi na Skaina Ally, Salma Jabu ‘Nisha’, Shamsa Ford, Starlisha Tillya ‘Chagga Baby’ na Siwema Edson ambaye pia alizaa naye mtoto mmoja.
auntezekiel4AUNT EZEKIEL
Ni staa wa filamu za Kibongo ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja, historia inamuonesha kama binti aliyewahi kuolewa mara mbili.
Aunt amewahi kuwa kwenye uhusiano na wanaume tofauti akiwemo Jack Pemba, Sunday Demonte, mwanaume anayetambulika kwa jina moja la Joff, Mwilu Mwilola ‘Silva’, Hatman Mbilinyi na Mnenguaji wa Diamond, Moze Iyobo ambaye ndiye baba wa mtoto wake.
wolpaJACQUELINE WOLPER
Mrembo mwingine kutoka Bongo Muvi ambaye amewahi kuripotiwa kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo Ramadhan Mtoro ‘Dallas’, Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Mwami Rajabu mwenye asili ya Kongo, Ababuu ambaye ni marehemu kwa sasa na Mkongo anayeishi naye kwa sasa.
vincent kigosiVINCENT KIGOSI ‘RAY’
Ni mmoja wa wasanii wa filamu Bongo ambaye anaingia kwenye listi ya wanaume waliowabadili wanawake kama nguo. Kati ya wanawake hao ni Blandina Chagula ‘Johari’, Ruth Suka ‘Mainda’, Chuchu Hans na wengineo.
wemaWEMA SEPETU
Huenda ndiye staa wa kike mwenye historia ya kuwabadili wanaume, hasa mastaa kuliko wengine wote. Akiwa ni muigizaji mwenye uwezo mkubwa, Wema anatajwa kuwahi kutoka na TID, Mr Blue, Chalz Baba, Steven Kanumba, Diamond Platnumz, CK, Mkongo na Idris Sultan.
kajala 1KAJALA MASANJA
Mkali huyu wa filamu za Kibongo, naye anaingia katika orodha hii, akidaiwa kutoka na wanaume wengi kwa nyakati tofauti.
Baadhi yao ni P Funky (baba mtoto wake), Faraja Chambo (aliyekuwa mumewe), Quick Rocka, Diamond, Kigogo wa ikulu na wengineo.
SIYO FRESHI, SIYO POA!
Ingawa kila mtu ana maisha yake, lakini safu hii inaamini kwamba siyo fresh wala siyo poa kabisa kwa mastaa ambao ni vioo vya jamii, kuwa na tabia ya kubadilisha wapenzi kila mara.
Mtu unaweza kulazimika kubadili mtu uliyenaye, lakini hiyo ni lazima kuwepo na sababu ya msingi inayokusukuma kuchukua uamuzi huo, si kufanya hivyo kwa sababu tu una jina kubwa au una fedha za kutosha.