Akipiga stori na paparazi wetu, Mdidi alisema wakati Wastara anaolewa walihuzunika ila siyo kwamba hawakutaka aolewe bali ni kutokana na mazoea kwamba watakosa kuwa naye karibu.
“Madai ya talaka ya Wastara yameniumiza sana kwani tulikuwa tunatatarjia akishakaa vizuri kwenye ndoa tuendeleze Kampuni ya WAJEY lakini tangu ameolewa, mambo ni vululuvululu na hili la talaka nalo ndiyo linazidi kutuumiza,” alisema Mdidi.