Bondia Mfilipino, Manny Pacquiao amempiga Mmarekani Timothy Brandley katika pambano lao la tatu lililofanyika leo alfajiri katika ukumbi wa MMG, Grande Arena, Las Vegas nchini Marekani.
Majaji watatu wa pambano hilo wote walimpa Manny Pacquiao ushindi wa 116-110, hivyo kuwa Bingwa mpya wa Dunia wa uzito wa ‘Welterweight’ wa WBO.
Manny alimuangusha chini Brandley mara mbili katika pambano hilo, ikiwa ni katika raundi ya 7 na raundi ya 9.
Akizungumza baada ya pambano hilo, Pacquiao alikiri kuwa anaastafu masumbwi na sasa ataendelea na shughuli zake za kuwatumikia wananchi wa Ufilipino akiwa kama Mbunge wao.
“Ndio nastaafu,” alisema. “Nataka kwenda nyumbani kwa familia yangu na kuwatumikia watu wangu. Nawapenda mashabiki wangu na nawashukuru kwa ‘sapoti’ waliyonipa,” aliongeza.