Saturday, April 9, 2016

Tunda: Kupiga Picha Nusu utupu ni Hobi Yangu


MUUZA nyago Bongo, Tunda Sebastian amesema miongoni vya vitu ambavyo anajiona yuko huru kuvifanya ni kupiga picha za kihasara kwani anachukulia kama hobi yake.

Tunda alifunguka hayo baada ya kuulizwa sababu za yeye kupenda kupiga picha hizo ambapo alisema, yeye haoni tatizo katika hilo kwani hata wazazi wake walikuwa wakimpigia kelele lakini sasa wametulia.

“Huwezi kumjaji mtu kwa picha, sioni tatizo kwani hata ‘home’ wanajua kuwa hiyo ni hobi yangu,” alisema Tunda huku wengi wakimponda kwa tabia hiyo chafu inayokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania