Tuesday, April 5, 2016

VIDEO: Wezi Wa Laptop Kwenye Magari Wanalostisha Sana… Tazama Walichowafanyia Kina Master J Kwa Sugu

April 4 2016 Msanii wa HipHop Joseph Mbilinyi (Mr II Sugu) ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini aliwakutanisha mastaa wa bongofleva akiwemo Producer Master J, ni kwenye shooting ya video yake mpya ya Freedom inayofanywa na director Hanscana ndipo wezi walipovamia baadhi ya magari na kufanya wizi.
Location yenyewe kunakotengenezwa video hii ni nje kabisa ya jiji la Dar es salaam, panaitwa Ununio…. ni eneo ambalo huwezi kutegemea huo wizi kufanyika maana tulishazoea wizi kama huu unafanyika sehemu zenye watu wengi au pilika za hapa na pale zipo nyingi tofauti na Ununio.
Sio gari la Master J pekee lililovunjwa, yamevunjwa magari ya watu wengine pia waliokua wamekusanyika kwa ajili ya utengenezaji wa video hii.