Sunday, April 10, 2016

Video:Niliumia Kumuona Wema Akimbusu Mwanaume Mwingine-Idrissa


12446365_1699268810331221_476709445_n
Idris na mtangazaji wa The Trend, Larry Madowo

Akiongea kwenye kipindi cha The Trend cha NTV ya Kenya, Idris alisema ‘hicho ni kitu kibaya zaidi kuwahi kumtokea.’

“Ingetokea kwamba tupo kwenye party na kuna huyu jamaa ‘gay’ najua wakati mwingine ni kitu cha mchezo kumbusu mwanaume ‘gay’ haijalishi, wao ni nyoka wasio na sumu lakini inapotokea unapuuzia tu,” amesema.
“Lakini pale video inapowekwa mtandaoni na kila mtu anaiongelea na kila mtu anakuja kwangu kusema ‘mwanamke wako anachukuliwa tu na huwezi kufanya chochote, sasa wanaanza kuniita bwege na vitu kama hivyo, huwezi hata kumtawala mwanamke wako, huwezi hata kumkataza kufanya hili na lile na ninapoongea naye hanijibu vizuri,” alisisiza.
“Niliongea naye na akaniletea kiburi, alipokuwa hivyo nikasema nilitarajia walau ungeelewa, sijisikii vizuri kuhusu hili. Ninajisikia vibaya si kuhusu busu lenyewe ni kuhusu kwanini ipo mtandaoni, ni chuki kiasi gani ninazopata kutokana na hili, hakuwa anapata chuki kama niliyokuwa napata kwasababu ya video hiyo. Baada ya kusema nimechoka na kutoheshimiwa, watu ndio wakaelewa kuwa Idris anakuwa mwanaume wakati mwanzoni walisema ‘anakuwa kama mwanamke sasa’ kwasababu nini mwanamke wake anachofanya,” aliongeza Idris.
Idris anadai kuwa mwanzo alipoona video hiyo alidhani ni utani wa siku ya wajinga duniani. “Na kisha nikagundua kuwa huu si utani wa siku ya wajinga, hii inaumiza,” anasema.
“Ingekuwa mimi video yangu imesambaa nambusu mwanamke msagaji hakuna mtu angejali, watu wangapi wanajua kuwa labda jamaa huyo ni ‘gay’ au sio, hakuna anayejua.”
Idris amesema hawana maelewano mazuri na Wema kwa sasa kutokana na video hiyo.