MTANDAO maarufu wa kuweka video mbalimbali, Youtube umempa ‘big up’ msanii anayekuja kwa kasi kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajabu Abdulkhali ‘Harmonize’ kwa kuweza kufikisha watazamaji milioni mbili ndani ya siku 29 kupitia wimbo wake wa Bado.
Katika mtandao huo, ulionesha kushangazwa na msanii huyo kutoka Afrika Mashariki ambaye katika wimbo huo ameshirikiana na bosi wake, Diamond Platnumz.
“Ajabu!! Video hii ya muziki kutoka Africa Mashariki kufikisha idadi ya watazamaji Youtube milioni mbili ndani ya siku 29,” uliandika mtandao huo.
“Ajabu!! Video hii ya muziki kutoka Africa Mashariki kufikisha idadi ya watazamaji Youtube milioni mbili ndani ya siku 29,” uliandika mtandao huo.
Akizungumzia ishu hiyo, Harmonize alisema;
“Ni suala la kumshukuru Mungu na mashabiki wanaonisapoti lakini pia Diamond kwa mchango wake mkubwa wa kuamua kushirikiana na mimi.”
“Ni suala la kumshukuru Mungu na mashabiki wanaonisapoti lakini pia Diamond kwa mchango wake mkubwa wa kuamua kushirikiana na mimi.”