Thursday, May 5, 2016

Audio ya SHILOLE juu ya Msanii mwenzie SNURA kufungiwa na nyimbo ya CHURA kufungiwa


Ni Mei 4, 2016 ambapo kupitia wizara ya Habari na Utamaduni, Michezo walitoa taarifa za kuufungia wimbo wa Snura ‘chura’ kuchezwa kuanzia leo na kuitoa nyimbo hiyo kwenye mitandao yote ya kijamii mpaka hapo Snura atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo. 
Sasa taarifa hizo zimemfikia Soudy Brown wa U Heard wa kipindi cha XXL ambapo kwenye Uheard amesikika Snura alichowahi kuzungumza kabla ya ngoma yake kufungiwa "siruhusu video yangu kuchezwa kwenye TV yoyote, ile video ni ya youtube kwa hiyo mtu anaposema maadili, sijui watoto, huyo mtoto anayeacha kwenda library kujisomea na kutafuta chura youtube huyo ni mtu mzima’"
Soudy Brown amezungumza na Shilole na kumuuliza kama amesikia wimbo wa ‘Chura’ kufungiwa, Shilole ameyazungumza haya "nimezisoma habari hizo japo sijazijua kwa undani, mimi nampa pole tu lakini ndio tujifunze kupitia vitu kama hivi"
Bonyeza play kuisikiliza story yote iko hapa