Sunday, June 19, 2016

Makachero Watumwa Mwanza na Arusha Kuchunguza Mauaji ya dada wa bilionea Msuya

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam limetuma timu ya maofisa wake kwenda mikoa ya Arusha na Mwanza kufanya upelelezi wa mauaji ya dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.

Hadi sasa jeshi hilo limewakamata watu wanne kwa tuhuma za mauaji hayo, akiwamo mumewe Aneth, mfanyakazi wao wa ndani na hawara wa mfanyakazi huyo.

Kamanda Sirro hakumtaja mtuhumiwa wa nne aliyekamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo yaliyogusa hisia za watu.

Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojuliana Mei 26 mwaka huu, nyumbani kwake Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao inadaiwa hawakuchukua kitu chochote ndani na kutoweka.

Sirro alisema alituma maofisa hao kwenda Mwanza na Arusha kufanya upelelezi wa mauaji ya Aneth ili kubaini chanzo chake.

Hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi sababu za kutuma timu hiyo kwenye mikoa hiyo wakati mauaji hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam.

“Jeshi la polisi bado tunafuatilia, kwa sasa tumeshatuma maofisa wetu wameenda katika mkoa wa Mwanza na Arusha ili kufanya upelelezi zaidi,”alisema Sirro.

Alisema jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa wanaowashikilia ili kubaini chanzo cha mauaji hayo, hivyo upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 12 na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kandokando ya barabara eneo la Mojohoroni wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro.

Februari 10, mawakili wanaosimamia kesi ya bilionea huyo, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu, waliiambia mahakama kuwa Serikali inakusudia kuita mashahidi 50 kuthibitisha mashtaka na kuwasilisha vielelezo 40, ikiwamo bunduki iliyotumika katika mauaji hayo.

Mawakili hao walidai mipango ya kumuua bilionea Msuya ilianza Julai 26, mwaka 2013 jijini Arusha, ikiwahusisha washtakiwa hao baada ya kuahidiwa wangelipwa Sh5 milioni kila mmoja.

Makonda Kupiga Marufuku Uvutaji Sigara Hadharani

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema waendesha bodaboda na abiria wasiovaa helmet watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua.

Makonda aliyemwakilisha Makamu wa Rais kwenye futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wateja na wadau wake juzi, alisema abiria na wapanda vyombo hivyo wanatakiwa kuvaa helmet.

Alisema kupanda pikipiki bila usalama ni kwamba abiria anadhamiria kujiua, kwa sababu akipata ajali ni rahisi kupoteza maisha kwa kupiga kichwa chini.

“Nimeshawasiliana na kamati yangu ya usalama barabarani mkoa, hili nitalisimamia kikamilifu lazima wote wawe na helmet na wakikamatwa wote watashtakiwa,” alisema.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kupanda bodaboda bila kuvaa kofia hiyo, ni sawa na mtu anayechukua vidonge na kunywa na pombe kali, ambayo matokeo yake ni kifo.

Makonda alisema kazi hiyo ataifanya kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani ili apate thawabu ikiwamo kuruhusu maduka makubwa kufanya kazi hadi usiku wa manane.

Alisema hiyo itasaidia wanaofanya kazi wakirudi nyumbani wanafuturu baadaye wanaswali Tarawehe, hivyo wanaweza kwenda kufanya manunuzi usiku.

Alisema kitakachofanyika ni kuimarisha usalama wa raia kupitia kamati yake ya ulinzi na usalama ya mkoa.

Pia, alisema atatangaza kupiga marufuku uvutaji sigara hadharani zaidi kwenye mikusanyiko na kupambana na vijana na watu wanaojihusisha na uvutaji wa shisha (bangi).

“Mtu asiyevuta sigara, anakerwa sana na moshi ndiye anayeathirika zaidi, nitatangaza rasmi hivi karibuni marufuku ya kuvuta sigara, sasa watu watafute kwa kuvutia… nitatangaza na hatua za kuchukua,” alisema.

Makonda alitumia nafasi hiyo kuwataka NMB kuchangia madawati, kwa shule za msingi na sekondari katika mkoa wake.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker alisema utamaduni wa kufuturu pamoja hasa katika Afrika unadumisha amani, umoja na upendo miongoni mwa Waislamu na watu wengine, hivyo wao wanauendeleza.

Ommy Dimpoz: "Ndoa ya Mwana FA Haikuwa ya Kifahari Lakini Bora Kuliko Nyingi Nilizowahi Kuhudhuria"

Ndoa ya Mwana FA haikuwa ya kifahari lakini ilikuwa bora, yenye furaha na iliyochangamka kuliko nyingi nilizowahi kuhudhuria, Ommy Dimpoz.

Akizungumza kwenye documentary yangu maalum niliyoipa jina ‘Bado Nipo Nipo ilivyogeuka kuwa historia kwa Mwana FA’, Ommy amedai kujifunza mengi kupitia ndoa ya swahiba wake huyo. 

FA alifunga ndoa June 5, 2016 na mchumba wake wa miaka mingi ambaye tayari pamoja wana mtoto wa kike aitwaye Maleeka.

“Watu wengi wanaogopa kuoa kwasababu ya kufikiria gharama, naweza kusema kwamba ndoa ya Mwana FA haikuwa ndoa yenye mambo ya kifahari lakini ilikuwa moja ya ndoa nzuri kabisa nilizowahi kuhudhuria,” anasema Ommy.

“Haikuwa na mambo mengi kwa maana ya magharama, tumetoka msikitini tumeenda moja kwa moja nyumbani kwake. Baada ya hapo nyumbani kulikuwa tu na kasherehe kadogo tumekusanyika washkaji, kama house party. Ukiangalia kwasababu ilikuwa ndoa ya staa ikawa kubwa,” ameongeza.

Ommy pia amedai kuwa FA alikuwa amepanga kuifanya ndoa itakayohusisha watu wachache sana na ya faragha.
“Mwenyewe alitaka kwamba harusi iwe ni ya watu wasiozidi kumi,” anasema. 

“Hakutaka watu watu wajue kabisa. Tulikubaliana kwamba hakutakuwa na picha hata moja. Kwahiyo mimi nilikuwa nahisi naenda kwenye harusi ambayo sitapost chochote. Lakini nafika msikitini naona watu wako busy wanairekodi Snapchat… nikaona hapa hamna siri na mimi nikaanza kurekodi hapo hapo nikaanza kuzirusha.”

“Baada ya hapo unajua tena ndoa jambo la heri, sio jambo la siri.”

Dokta Atoboa Siri 8 Mimba za Wema Sepetu Kuyeyuka

Imevuja! Kuyeyuka au kuharibika kwa ule ujauzito wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ hivi karibuni kumetajwa na daktari kuwa ni matokeo ya tabia yake ya kukaidi ushauri wa kitaalam, Amani lina cha kuwapa wasomaji wake.

Hayo yalisemwa na mtu wa karibu we Wema (jina lipo) akizungumzia  masharti ambayo daktari aliyepata kumtibu mrembo huyo aliyasema. Lakini pia, daktari mwingine wa jijini Dar, Dk. Fadhili Emily naye ameibuka na kuliambia Amani kuwa, Wema ana sababu 8 za mimba zake kuyeyuka akiwa anajua au hajui.

DAKTARI WA KWANZA
Mtu huyo wa karibu na Wema alisema mimba ambayo staa huyo aliifanyia shoo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuyeyuka Februari, mwaka huu, ilitokana na sababu ya kugoma kutii masharti ya kitabibu.

SABABU YA KWANZA
“Vipimo vya kitabibu vilisema kuwa Wema alitakiwa kupumzika kwa muda mrefu ili kuilinda mimba hiyo kwani ilikuwa katika hatihati ya kutoka kama mhusika atakuwa ni mzururaji. Sasa Wema akiwa mjamzito alikuwa hakosi viwanja.”

USHAHIDI
Februari, mwaka huu, akiwa mjamzito, Wema alihudhuria tukio la uzinduzi wa Video ya Lupela iliyozinduliwa na Alikiba Salehe kwenye Hoteli ya Slipway, Oysterbay jijini Dar.

SABABU YA PILI
“Ilifika wakati, Wema alitakiwa kupewa bed rest (mapumziko ya kitandani) ili kulinda mimba yake. Hilo nalo likawa gumu kwake kukubaliana nalo. Ndiyo ikawa sababu ya mimba kutoka.”

SABABU YA TATU
“Sababu ya tatu, aliambiwa na daktari wake asifanye kazi ngumu, jambo ambalo lilikuwa likimshinda. Yeye si mtu wa kukubali kukaa tu muda wote. Hilo nalo lilichangia.”
Wema SepetuWema akiwa na mama yake mzazi

SABABU NYINGINE 5
Naye Dk. Fadhili, akizungumza na gazeti hili Jumatatu iliyopita, alisema sababu tatu ambazo zinadaiwa zilichangia mimba ya Wema kuyeyuka ni za kweli, lakini akasema Wema bila kujijua au akijua, mimba zake kadhaa zimeshatoka kwa vile wanawake wengi wenye matatizo ya kutoshika mimba, hushika na kutoka bila wenyewe  kujijua na pia akaanika sababu za hali hiyo kumtokea mwanamke.

Lakini akasisitiza kuwa kuharibika kwa mimba ni tatizo ambalo linaweza kumkumba mwanamke yeyote, si Wema tu.

SABABU ZA KIMAUMBILE
“Sababu za mimba kutoka zenyewe zinatajwa kwamba ni tabia ya kurithi, yaani vinasaba ambavyo si vya kawaida. Kwa hiyo, kiumbe kinakuwa katika hali ambayo kwa asili mimba haiwezi kukua.  Kama mtoto akizaliwa basi atakuwa na matatizo ya kimaumbile na kiakili.”

SABABU YA MUUNGANO
“Sababu nyingine ni kukosekana kwa yai lililorutubishwa.  Katika kuumba, yai la mwanamke hukutana na mbegu ya mwanaume na zoezi la kiumbe kukua huanzia hapo kwa yai kujitenga mara mbili.  Upande mmoja hutengeneza kondo la nyuma na kifuko cha kutunza maji na sehemu ya pili hutengeneza kiumbe au mtoto.

“Huwa inatokea sehemu ya kondo la nyuma inaendelea kukua wakati sehemu ya mtoto haikui. Katika hali kama hii, kama mama hajafanya vipimo kujua maendeleo ya mtoto, uwezekano wa mimba kutoka kabla ya kufikisha wiki 24 ni mkubwa.

“Lakini hili la muunganiko nasema pia kwamba, kwa mwanamke ambaye mimba yake inahofiwa kutoka, ni hatari kuendelea kukutana kimwili na mwanaume wake kwani uwezekano wa kutoka ni mkubwa.”

KUHUSU IDRIS
Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba walikuwa wakiendelea ‘kukutana’, lakini kipindi cha ujauzito wake, Wema na Mbig Brother, Idris Sultan uhusiano wao ulikuwa umekolea.

SABABU YA POMBE
“Sababu nyingine inayochangia kuharibika kwa mimba ni unywaji wa pombe kupita kiasi kwa mama mjamzito au kuvuta sana sigara,” alisema dokta huyo.

SABABU YA MAGONJWA
Sababu nyingine alizitaja kuwa ni magonjwa yanayoshambulia mwili wa mama na kiumbe wake tumboni kama vile malaria na kaswende.

SABABU YA KUTOA MIMBA
Daktari huyo alisema kuwa, mwanamke kutoa mimba mara kwa mara kunachangia kuharibika au kushindwa kunasa mimba baadaye.

“Lakini si lazima awe anatoa mimba mara kwa mara, mwanamke anaweza kutoa mimba mara moja tu ikiwa katika mazingira ya ukuaji salama. Hilo linaweza kuwa tatizo kubwa la mimba kutoka siku za usoni,” alisema.

USHAHIDI
Katika mahojiano na gazeti damu moja na hili, Risasi Jumatano mwaka jana, Wema alikiri kuwahi kutoa mimba moja tu ya aliyekuwa staa wa filamu za Bongo, marehemu Steven Kanumba.

WEMA ASAKWA
Mpaka juzi Jumanne, gazeti hili lilikuwa limetimiza siku saba za kumsaka Wema kwa ajili ya kupata vielelezo vyake kufuatia madai au maelekezo hayo ya daktari lakini bila mafanikio kwani hapokei simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, nao hakuujibu

Chanzo:GPL

Video ya Aibu ya Wema Sepetu Yavuja!

 Video ya aibu inayomuonesha msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ akicheza kihasara mbele ya mwanaume imevuja, Risasi Jumamosi linayo kibindoni.

‘Klipu’ hiyo ambayo Wema anaonekana akikata mauno huku suruali aliyokuwa amevaa ikimvuka na kuacha wazi sehemu ya makalio yake, ilivujishwa hivi karibuni na mdau mmoja wa burudani ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

“Hii video niliichukua siku ya ile eventi ya Christian Bella ya kutimiza miaka 10 pale Escape One. Wakati akicheza na msanii wa Kundi la Pah One aitwaye Igwe, Wema alionekana kama alikuwa amelewa, alikuwa akikata mauno lakini aibu zaidi ilikuwa pale ambapo ile suruali yake ilipomvuka na sehemu ya makalio yake kubaki wazi.


“Sidhani kama alikuwa kavaa kufuli, baadhi ya watu waliokuwa wakimkodolea macho walishindwa kuamini kama ni Wema yule wanayemjua,” alisema mnyetishaji huyo.
Baada ya mwandishi wetu kupata nafasi ya kuiangalia mwanzo mpaka mwisho, alijiridhisha kuwa aliyekuwa akionekana kwenye video hiyo ni Wema na kweli alichokuwa akifanya ni aibu tupu.

Aibu yake ni pale ambapo suruali inamvuka na kuacha sehemu zake za siri wazi lakini pia staili ya kumkatikia msanii aliyekuwa akicheza naye kwani jamaa alikuwa ‘akikamatia chini’ huku naye akionekana kutokwa na udenda.

Paparazi wetu alijaribu kumtafuta Wema ili kuizungumzia ‘klipu’ hiyo lakini simu yake kila ilipopigwa ilikuwa haipokelewi.

Chanzo:GPL

Baada ya TCRA Kuzima Simu Feki, Wafanyabiashara Wamepata Soko Jipya la Simu Hizo


Moja ya habari iliyoripotiwa ni hii kutoka gazeti la Mwananchi, yenye kichwa cha habari ‘simu bandia zapata soko Msumbiji, Congo’.

Gazeti hilo limeripoti kuwa Siku mbili baada ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima simu feki, wafanyabiashara wa simu hizo wamepata soko jipya katika nchi za Msumbiji na Congo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hilo, baadhi ya vijana waliokutwa wakizunguka madukani kuzikusanya, walisema wanazinunua na kuzisafirisha kwenda huko kwa ajili ya kuziuza kwa watumiaji. Walisema katika nchi hizo kuna soko kwa sababu zinakamata mawasiliano kama kawaida.

Gazeti hilo limemnukuu Lawrence Kyondo ambapo amesema wanazinunua kwa bei ya makubaliano na kwenda kuziuza katika soko la nje……….>>>’hatujaanza hii biashara leo, siku nyingi isipokuwa wenye maduka walikuwa bado wagumu kuziuza wakidhani hazitazimwa’

Utameza Mate Kama Fisi! See What This Naughty Swahili LADY was Doing in Private (VIDEO)

Forget about Wadada wa Mjini and their fake dancing styles, Swahili ladies are the real deal.
They have mastered the skills of teasing men with seductive dance moves that leave little to one’s imagination.

See what this hot Swahili lady was doing in her house. 

Dakika 90 za Mchezo wa Mpira Zinanichosha - Wema Sepetu

Muigizaji Wema Sepetu, amesema mchezo wa soka unamchosha kuangalia kwa kuwa unatumia muda mrefu wa dakika 90 huku wachezaji wake wakihangaika mno kutafuta mabao tofauti na mpira wa kikapu (Basketball).

Wema anasema mara nyingi akiwa nyumbani kwake hupenda kuangalia mpira wa kikapu kwani hauchoshi na wachezaji huwa wanatumia muda mfupi kupachia mabao.
Ili aangalie soka na kumaliza muda wote wa mchezo ni lazima awe na kampani yake na mara nyingi iwe laivu uwanjani

Irene Uwoya na Skendo ya Kubakwa!

Untold story! Skendo ambayo haijawahi kuandikwa wala kusimuliwa popote inayomhusu mwigizaji ‘hot’ wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krish’ ni juu ya madai ya kubakwa na mfanyabiashara maarufu wa Kihindi jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa), alipokuwa na umri wa miaka 18 ambapo kwa sasa ana umri wa miaka 28, Ijumaa limefukunyua na kuinyaka.

Chanzo chetu makini ambacho ni mtu wa karibu wa Uwoya kilichoomba hifadhi ya jina gazetini kilidai kuwa, tukio hilo limekuwa likimtesa Uwoya kwenye maisha yake kiasi kwamba kila akilikumbuka huwa anakosa amani.

KISIKIE CHANZO
“Irene (Uwoya) ana kitu ambacho kinamtesa sana na mara kadhaa amekuwa akiniambia kuwa, ipo siku atakitengenezea filamu, anazungukazunguka sana ila alimdokeza mtu kuwa aliwahi kunusurika kubakwa, labda mkijaribu kumdodosa anaweza kuwapa ukweli,” kilifunguka chanzo hicho na kuongeza:

“Chondechonde asijue tu kwamba mimi ndiye nimewaambia maana alisema skendo hiyo ikiandikwa magazetini na dunia ikajua kilichompata, anaweza akajifungia ndani mwaka mzima kwa aibu.”

UWOYA ANASEMAJE?
Baada ya kuinasa habari hiyo, Ijumaa lilifanya jitihada za makusudi za kumsaka mlimbwende huyo aliyeshiriki Shindano la Miss Tanzania 2006/07 na kushika nafasi ya tano ambapo baada ya kubanwa ipasavyo kwa kuwa alikuwa hataki kusikia habari hiyo, alikiri kunusa skendo hiyo ila akafafanua kuwa, si kweli kwamba alibakwa bali ilibaki ‘kiduchu’ kitendo hicho kikamilike.

“Nikiri tu kwamba ni tukio ambalo sijawahi kulisimulia popote lakini kwa kuwa umenibana, ngoja niseme kilichotokea ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema Uwoya na kuendelea:

“Sikumbuki ilikuwa mwaka gani ila ni kweli nilikuwa na kama miaka 18. Nilikuwa na tabia ya kwenda na wenzangu kwenye nyumba ya mfanyabiashara mmoja ambaye alikuwa jirani yetu, Mbezi- Beach (naomba nisimtaje) kuangalia muvi.

“Siku moja, tukiwa kwenye sebule ya tajiri huyo ambaye ana asili ya Kihindi aliyekuwa akiishi peke yake, aliniita chumbani kwake.

“Kwa kuwa tulikuwa tumezoeana sana, sikuwa na wasiwasi wala kudhani angeweza kunifanyia jambo baya. Hee! Ile kuingia ndani si akafunga mlango, wenzangu kule sebuleni hawakujua chochote. Alichokifanya ni kunilazimisha kufanya naye mapenzi kwa nguvu, akaanza kunivua nguo, nikaona hapa nimekwisha.

“Nilichokifanya nilipiga kelele huku nikipiga ule mlango ndipo wale wenzangu walipokuja na kutaka mlango ufunguliwe, jamaa alipoona kimenuka alifungua mlango akatoka nduki na kutokomea nje.”

TAARIFA YAFIKA KWA WAZAZI
Kufuatia tukio hilo, Uwoya alifikisha taarifa kwa wazazi wake ambapo baba yake, Mzee Pancras Uwoya alilivalia njuga na kumfungulia kesi mfanyabiashara huyo, kesi ambayo ilinguruma kwa muda mrefu.

“Ni tukio ambalo liliwashangaza wengi na sikumbuki hasa kilichoendelea ila ninachojua yule mfanyabiashara alitoa fedha nyingi kwa kitendo kile cha kunidhalilisha,” alifunguka Uwoya.

ANAFICHA KUBAKWA?
Alipobanwa juu ya madai kuwa alibakwa ila hataki watu wajue kuwa alifanyiwa kitendo hicho, Uwoya alisema: “Kwa kweli hakufanikisha azma yake, alilazimisha kunivua nguo kweli lakini hakufanikiwa baada ya mimi kupiga kelele.

KWA NINI AMEFUNGUKA LEO?
“Nimeamua kuliweka wazi kwa kuwa umenibana juu ya ishu hiyo na ili watu wajue kwamba sijawahi kukwaa skendo ya kubakwa ‘pasee’ ila nilinusurika kubakwa. Lakini pia nimefanya hivi ili kuwapa fundisho wasichana wengine kutomuamini kila mtu, kwani aliyetaka kunifanyia kitendo hicho ni mtu ambaye sikumdhania.”

Jionee Mawaziri wa Sudan Kusini Wanavyovyaa

Kulia ni Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji huko Sudan Kusini bwana MABIOR GARANG (aliyevaa viatu vyeupe).

Katikati ni Waziri wa Ulinzi aliyevaa kandambili na utepe mwekundu begani,

Kushoto ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, aliyeshika kirungu nje ya ukumbi wa Bunge mjini Juba Sudan Kusini.

Magazeti ya Leo Jumapili ya June 19



Lowassa Atoboa Siri Ya Ujio wa TB Joshua Nchini.....Asema Aliitwa na CCM Kumshawishi Akubali Matokeo ya Uchaguzi Mkuu


Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa amesema hakuridhika na matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, na kwa kulijua hilo, ‘watawala’ walimleta rafiki yake kutoka Nigeria, TB Joshua ili amshawishi akubali matokeo. 

Lowassa alisema baada ya TB Joshua, muhubiri na kiongozi wa Synagogie Church of All Nations, kukaa naye pamoja na viongozi wengine wa Chadema na kumueleza jinsi ‘walivyoporwa’ ushindi, kiongozi huyo wa kidini alichukia na kusitisha azma yake ya kuhudhuria sherehe za kumuapisha Rais John Magufuli.

TB Joshua aliwasili nchini Novemba 3, siku mbili kabla ya kuapishwa kwa Magufuli kuwa Rais, na alienda Ikulu na baadaye nyumbani kwa Lowassa ambaye alitumia muda mwingi wa ziara yake pamoja naye. 

“Walimuita rafiki yangu TB Joshua, wakaenda wakampokea. Alipokelewa na Rais Magufuli, akapelekwa Ikulu akazungumza na Kikwete,” alisema Lowassa. 

“Baadaye akawaambia wamlete kwangu. Kweli akaja nyumbani kwangu, tukazungumza naye. Sitaki kusema mengi sana niliyomwambia, lakini moja, nilimwambia ukikubali yale matokeo ndugu yangu, heshima yako itashuka hapa nchini na duniani kwa ujumla,”alisema. 

Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Wafuasi wa Chadema (Chaso) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 

Alisema ni kutokana na msimamo na mazungumzo waliyofanya na TB Joshua ndio yaliyosababisha kiongozi huyo wa kidini maarufu barani Afrika kutohudhuria sherehe hizo za kuapishwa zilizofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Katika hotuba yake, Lowassa alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada anazozichukua za kujaribu kufufua uchumi wa nchi, lakini akasema hakubaliani na mbinu anazotumia. 

Alisema anafurahia kumsikia Rais Magufuli akiihubiri nchi ya viwanda, lakini hana imani na lugha anazotumia.

“Rafiki zangu nawasikia na nafurahi sana wanasema wanataka kujenga nchi ya viwanda. Natamani nchi hiyo, lakini lugha hiyo sina imani nayo sana,” alisema. 

Alisema haziamini lugha hizo kwa kuwa ni vitu visivyowezekana kutokana na ukweli kuwa viwanda vilivyopo haviwezi kufufuka na kuondoa tatizo la ajira lililopo nchini. 

“Wanasema watafufua viwanda, lakini viwanda vilivyopo vili kuwa analojia sasa hivi mambo yote ni ‘digital’. Hicho kiwanda kitafufuliwaje maana hata madukani spea zake hazipo labda zitengenezwe upya,”alisema. 

Alisema tatizo lililopo kwa sasa nchini ni la ajira na kwamba hata kaulimbiu yao kwenye kampeni ilikuwa ajira kwa kutambua kuwa wapo vijana wengi waliomaliza vyuo, hawana ajira na kwamba eneo kubwa litakaloweza kuwaajiri ni sekta ya kilimo. 

Lowassa, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, alisema anakubaliana na kauli iliyotolewa na Jenerali Ulimwengu aliyoitoa hivi karibuni kuwa Rais Magufuli ameturudisha nyuma miaka 50, akiponda uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja. 

“Uamuzi ule si mzuri na una matatizo makubwa kwa kuwa ni kuwanyima wananchi haki yao muhimu ya kuwasikiliza wawakilishi wao,” alisema.

Akizungumzia elimu, Lowassa alisema wakati Chadema na Ukawa waliposema watatoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu walikuwa wamejipanga, lakini Serikali imebeba sera hiyo bila kujiandaa.

Aliwapongeza vijana kwa kuwa kiini cha mabadiliko na kusema mpaka sasa akikutana na watoto wadogo wanamsalimia kwa kumwambia “Mabadiliko Lowassa”. 

Alisema vijana walifanya kampeni nzuri na kumwezesha kupata kura nyingi zilizowapa ushindi, lakini wakanyimwa ushindi. 

“Tulishinda vizuri sana lakini hata hizo walizotupa, zinatosha kuwaambia kuwa tuliwapa kazi ya kutosha. Nyie mnajua, wao wanajua na mimi najua,” alisema. 

Lubuva aondolewe 
Alisema licha ya kumuheshimu mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, anapaswa kutimuliwa kwa kushindwa kuisimamia vyema tume hiyo. 

“Tume ya Uchaguzi inapaswa iondoke. It must go na ndio maana nasema iko haja ya kuanza upya kudai Katiba mpya haraka iwezekanavyo,” alisema Lowassa. 

“Kama yupo mtu yeyote anayechukia matokeo ya uchaguzi uliopita, suluhisho lake ni kuwa na tume huru ya Uchaguzi itakayotokana na Katiba mpya. Tusipohangaika na Katiba mpya tutarudi palepale.”

Alirudia kauli yake kuwa baada ya uchaguzi kulikuwa na waliomtaka atangaze “kuingia barabarani”, lakini aliwakatalia. 

“Tutakuwa tunakwenda Ikulu kwa kufagia barabarani kwa damu za watu. No, tutakwenda Ikulu bila damu za watu wakati wowote na Mungu atatusaidia. Nawaambia wale wote ambao hawakuridhika, mnajua nguvu ya umma lakini msiitumie kuwaumiza watu,” alisema. 

Aliwataka viongozi wote wa Chadema kujali maslahi ya wanyonge kwa kuepuka kufanya kazi kwa mazoea. 

Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambaye ni diwani wa Chadema, Charles Mwita aliwataka wanafunzi kufanya kazi ya kukijenga chama kwani mabadiliko ya kweli yataletwa na vijana. 

Muasisi wa Chaso, Pamela Maasaio aliwataka vijana wa Chadema kuachana na siasa za kwenye mitandao na badala yake waende mitaani kupiga kelele na kuweka mikakati ya pamoja.