Wednesday, May 28, 2014

AUNT EZEKIEL USO KWA USO NA MBAYA WAKE CHINA..ALIYE MCHANA NA CHUPA KWA KUGOMBANIA BWANA..SOMA ZAIDI

MSANII wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amesema hivi karibuni aligongana uso kwa uso na Ivon Bigilwa ambaye anadaiwa kumchana kwa chupa mkononi na kesi hiyo inaendelea katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Msanii wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel akliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
 Aunty alisema hayo juzi Jumatatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya hakimu Agustina Mbando, akikanusha taarifa ya wadhamini wa Ivon, Christopher Mwaseba na Anthon Mwaseba walioiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alikuwa nyumbani akimuuguza mama yake.

Ivon Bigilwa aliyemchana Aunt kwa chupa.
 Msanii huyo alisema wadhamini hao wanaidanganya mahakama kwa kuwa hivi karibuni alikuwa nchini China na aligongana naye uso kwa uso.

Kutokana na hilo, Hakimu Mbando aliwaonya wadhamini hao kwa kuidanganya mahakama na kuwataka wampeleke mtuhumiwa huyo mbele ya mahakama
<<<<<BOFYA HAPA KUONA KURASA ZA MWANZO NA MWISHO ZA MAGAZETI YA LEO>>>>>