Mpango mzima wa kuwamwaga ‘minoti’ uliongozwa na muigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Jacob Steven ‘JB’, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wengineo ambapo mwishoni hesabu ya jumla ilitimia shilingi milioni tatu.
Kwenye sherehe hiyo, hawakuonesha utengano, hawakujali kama ni memba wa Bongo Movie au Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) lililowakilishwa na rais wake, Simon Mwakifamba ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.
Paul Mtenda akiwa na 'mai waifu wake' Vanitha.
Mbali na Steve Nyerere, JB, Batuli na Dude, mastaa wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Issa Mussa ’Cloud 112’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, William Mtitu, Single Mtambalike ‘Rich’, Yvonney Cherry ‘Monalisa’, Suzan Lewis ‘Natasha’ na wengine wengi.<<<<KISA POMBE..HUYU MREMBO KAANIKA UTAMU WAKE HADHARANI..BOFYA HAPA KUMUONA>>>>