Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati jijini Dar, Aunt alidai kuwa alikerwa na jambo hilo na kujikuta akishindwa kujizuia na kuwawakia kuwa hajaolewa na ndugu hivyo mwenye mamlaka ya kutoa talaka ni mumewe pekee.
Aunt alisema kwamba, amekuwa akisikia mara kwa mara habari za ndugu wa Demonte wakiongea maneno mengi ya kumfitinisha na mumewe.
Alidai naye ni binadamu hivyo jambo hilo limekuwa likimkera kwa sababu wanaongea maneno hayo pembeni na kwamba hakuna hata mmoja aliyewahi kumfuata na kumwambia juu ya suala hilo, zaidi amekuwa akiambiwa na watu wengine tu.
Akifafanua zaidi, Aunt alisema kwamba anawashangaa hao wanaojiita ndugu wa Demonte kuendelea kumtolea maneno ya kejeli kila kukicha na wakati kama wanahisi kuna tatizo kati yake na mumewe wangeweza kumtafuta na kuzungumza naye.
Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Demonte siku ya ndoa yao.
Alitiririka kuwa jambo ambalo halimpendezi ni pale anapokutana na watu wakimtuhumu kwamba eti ndugu wa mumewe wanataka kumpatia talaka.“Ujue hao ndugu wanaotaka kunipa talaka wanatakiwa waelewe kuwa mimi sijaolewa na wao, hivyo hata jukumu la kunipa talaka siyo lao, maana niko vizuri na mume wangu, wala hatujawahi kukwaruzana hata kuambiana ishu za kupeana talaka,” alisema Aunt.
Ndoa ya Aunt imekuwa ikisengenywa tangu ilipofungwa mwezi June, 2012 kufutia staa huyo kutoishi pamoja na mumewe ambaye inasemekana anaishi Dubai.