MWIGIZAJI wa Bongo Movies, Salim Ahmed ‘Gabo’ amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Kiwalani jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo makini, Gabo aliyekuwa katika gari binafsi, aligongana na gari lingine na kupata jeraha mguuni hivyo kulazimika kulazwa kwa takriban wiki tatu kisha kuruhisiwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza na paparazi wetu baada ya kutoka hospitali, Gabo aliyeitendea haki Sinema ya Majanga ya Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, alieleza mazingira ya ajali.
“Nilikuwa naendeshwa na rafiki yangu lakini ghafla tukagongana uso kwa uso na gari lingine, nashukuru magari hayakuumia sana lakini mimi nililazwa kwa wiki tatu kutokana na jeraha nililolipata mguuni,” alisema Gabo.