Friday, May 16, 2014

Picha za mtoto aliyefariki baada ya kuangukiwa na Jiwe kubwa huko Ilemela Jijini Mwanza..!

dogo
Mtoto  mmoja  aliyefahamika  kwa  Jina  la  Malaika  Jackson  amefariki  dunia   baada  ya  kuangukiwa  na  Jiwe  kubwa  lililoporomoka wakati   baba  yake  akichimba  kokoto  katika  mlima  Giza, maarufu  kama  mlima  wa  Rada  uliopo  maeneo  ya  Kiseke, Wilaya  ya  Ilemela  mkoani  Mwanza
Kabla  ya  kufikwa  na  mauti  hayo, Mtoto  huyu  alikuwa   na  baba  yake  mzazi  aliyefahamika  kwa  jina  la  Jackson  Ismail, mama  yake  mzazi  na  mdogo  wake    wakipata  chakula  cha  mchana  baada  ya  kuponda  mawe  kutwa  nzima…..
Huyu  ni  baba  wa  mtoto, bwana  Jackson Ismail  akimwangalia  mwanae  kwa  uchungu…
Wangali  wakipata  chakula  hicho, baba  aliwahi  kumaliza  na  hivyo  kuendelea  na  kazi  hiyo  ya  kuponda  mawe   huku  mkewe  na  watoto   wakimalizia  kupata  chakula….
Wakati  bwana  Ismail  akiendelea  kuyaporomosha  mawe  hayo,ghafla  alisikia  mtikisiko  mkubwa  na  hivyo  kumtaka  mkewe  na  watoto  watoke  haraka…..Mama  akiwa  na  mtoto  mchanga  waliwahi  kunyanyuka  na  kutoka,lakini  kabla  binti  Malaika  mwenye  umri  wa  miaka  mitano  hajatoka, jiwe  kubwa  lilimuwahi  na  kumkandamiza  na  kumfanya  afariki  dunia  papo  hapo….
Eneo  la  Tukio
Mwili  wa  Marehemu  Malaika  Jackson…
 
Baadhi  ya  wananchi  wakiwa  eneo  la  tukio