Hatimae Rihanna ameamua kuifuta account yake ya Instagram baada ya Uongozi wa mtandao huo wa Instagram kumzuia kuweka picha zisizokuwa na maadili ikiwa ni ukiukwaji wa sheria za mtandao huo.
Rihanna |
Mwezi uliopita rihanna alipewa onyo na mtandao huo baada yakuweka picha mbaya ambazo ni kinyume na masharti ya mtandao huo "Terms and Conditions"
Inaonekana rihanna akaona hio sio ishu na hatimae ameamua kuifuta kabisa account yake na kuhamia twitter ambako anaweka picha zake kwa uhuru zaidi bila kuzuiwa..
Baada tu ya Kujitoa kwa rihanna kwenye instagram, Ilifunguliwa account nyingine iliyo sadikiwa kuwa ni ya rihanna ikiwa na jina la "Badgalriri_again"
bidada huyu amethibitisha kuwa account hiyo siyo yake kwa kuandika kwenye twitter na kusema Instagram account Badgalriri_again ni fake na sio yake.
“#PHAKE !!!! Let’s be clear, I do NOT have an IG account!” aliandika rihanna kwenye mtandao wa twitter
-bongotoday