Monday, June 30, 2014

BABY MADAHA: SIOLEWI KWA KUFUATA MKUMBO WA WATU WENGINE

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema anaishi katika staili ya kivyake hivyo kamwe hawezi kuolewa kwa kufuata mkumbo kama ilivyo kwa wasanii wengine.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’
 Akipiga stori na mwandishi wetu, Baby Madaha al\ikiri kuwa ana mchumba ambaye ni Joh Kairuki, anampenda sana ila katika suala la kufunga ndoa bado yupoyupo sana kwa sababu haolewi kwa kufuata mkumbo kwani amejifunza kupitia kwa walioolewa na kuachika.

‘Baby Madaha’ akiwa kwenye pozi.
 “Nitaolewa nitakapokuwa tayari siyo kwa kufuata mkumbo vinginevyo bora nibakie hivihivi kwa sababu pesa kwangu ndiyo kila kitu, mambo mengine yanafuata,” alisema.