Wednesday, July 16, 2014

MOTO WATEKETEZA NYUMBA TATU MWANANYAMALA


 


Picha tofauti zikionyesha moto ukiteketeza nyumba maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam


WAKAZI wa Mwananyamala katika Barabara ya Malanga, mkabala na Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, walikumbwa na balaa mchana huu baada ya nyumba tatu kuteketea kwa moto na kuunguza vitu vingi ndani yake na vingine kuibiwa na vibaka.
Chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo pia wananchi walililaumu Jeshi la Zimamoto (Fire) kwa kuchelewa kufika eneo la tukio. Video ya tukio hilo kuwajia hivi punde.