Monday, April 20, 2015

LULU APATA KASHFA MPYA!

WAKATI mwili wa bilionea Lusekelo Samson Mwandenga ‘Seki’ aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita ukitarajiwa kuzikwa leo mjini Dodoma, mitandao mbalimbali ya kijamii imempa kashfa staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa kumtaja kuwa alikuwa na uhusiano wa ‘kimalovee’ na marehemu huyo, Ijumaa Wikienda linakujuza.
Staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Seki ambaye alikuwa na urafiki mkubwa na mastaa mbalimbali wa Bongo Movies, alifariki dunia baada ya kuanguka nyumbani kwake Madale jijini Dar ikidaiwa kuwa alikuwa akitaka kumuokoa mwanaye aliyekuwa akianguka ndipo yeye akaangukia meza ya kioo na kumchana tumboni.
ALIKUFA AKIKIMBIZWA HOSPITALI
Hata hivyo, wakati akikimbizwa hospitalini jijini Dar, alivuja damu nyingi hali ambayo ilimsababishia umauti kabla ya kupatiwa huduma ya kwanza.
LULU AANZA KUTAJWA
Saa chache baada ya kifo hicho kutokea, mitandao tofauti ya kijamii ilianza kumtaja Lulu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na bilionea huyo kwa kumpa pole pasipo kuwa na uhakika kama ni kweli au la!
“Mh! Pole Lulu kwa kufiwa na mtu wako, jamani huyu mtoto ana bahati mbaya sana sijui ni nini,” alichangia mdau mmoja katika mtandao wa Instagram.
POLE ZAZIDI KUMIMINIKA
Kadiri muda ulivyozidi kwenda ndivyo wafuasi wengi wa mitandao ya kijamii walivyozidi kummwagia pole nyingi Lulu huku wengine wakikemea suala la kumhusisha Lulu na bilionea huyo bila kuwa na ushahidi.“Jamani mna uhakika gani kama Lulu na huyo marehemu walikuwa na uhusiano? Mnamchafua bure mtoto wa watu,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.
LULU AJIONDOA INSTAGRAM
Wakati watu wakiendelea kumhusisha kimapenzi na bilionea huyo kwa namna tofauti mtandaoni, ghafla Lulu alifuta akaunti yake ya Istagram hivyo kuwafanya wafuasi wa mtandao huo kushindwa kuona mwigizaji huyo ametoa tamko gani kuhusiana na kifo hicho.
Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga ‘Seki’ enzi za uhai. 
BETHIDEI YA LULU YAYEYUKA
Kama hiyo haitoshi, siku hiyo ya msiba (Alhamisi), Lulu alikuwa akiadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwake ambapo angetimiza miaka 20 lakini kutokana na sababu ambazo hazikuweza kufahamika mara moja, hakufanya sherehe hiyo.
LULU ANASEMAJE?
Juzi, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Lulu kwa njia ya simu kutaka kujua taarifa za yeye kuhusishwa na bilionea huyo pamoja na mambo mengine, Lulu alijibu kwa kifupi:Ijumaa Wikienda: “Lulu kwanza tumesikia unaumwa na umelazwa, ni kweli?”
Lulu: “Siyo kweli, mimi mbona nipo tu hapa nyumbani.”
Ijumaa Wikienda: “Kuna manenomaneno kuhusu kifo cha Seki, watu wanakusema vibaya mitandaoni. Je, unatoa tamkoa gani?”Lulu: “Sina tamko lolote.”
Ijumaa Wikienda: “Lakini ni mtu uliyekuwa unamfahamu au alikuwa mpenzi wako?”
Lulu: “Sina cha kusema mimi na sina tamko lolote.”Ijumaa Wikienda lilipojaribu kumbana kwa maswali zaidi kuhusiana kuwa na uhusiano na bilionea huyo, kutofanyika kwa bethidei yake na kufuta akaunti ya Instagram, Lulu hakuwa tayari kujibu lolote.
Marehemu Seki ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa madini, Arusha na Dar ameacha mke na watoto wawili.
Mwili wake ulitarajiwa kuagwa jana katika Kanisa la KKT, Wazo-Hill jijini Dar na kusafirishwa mjini Dodoma kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo.