Sunday, July 13, 2014

VIBONDE WA KOMBE LA DUNIA WAZIDI KUMALIZIA HASIRA KWA MADEMU ZAO...ULISTAAJABU YA RONALDO, SHANGAA YA FABREGAS SASA!

KIUNGO wa Hispania, Cesc Fabregas yuko kwenye matanuzi na mpenzi wake Danielle Semaan kabla ya kwenda kuanza maandalizi ya msimu mpya na klabu yake mpya, Chelsea.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ameposti picha katika ukurasa wake wa Instagram akifanya matanuzi na mpenzi wake huyo.
Na Semaan nays ameposti picha ikiwaonyesha akiwa na mpenzi wake huyo pampja na binti yao, Lia.

Wenyewe hao: Kiungo mpya wa Chelsea, Cesc Fabregas (kushoto) akiwa na mpenzi wake Danielle Semaan (kulia) mapumzikoni
Fabregas (left) with his girlfriend Danielle Semaan (right) and his daughter Lia (centre)
Fabregas (kushoto) na Danielle Semaan (kulia) wakiwa na binti yao, Lia (katikati)

Chelsea inatarajiwa kuanza maandalizi ya msimu mpya mwanzoni mwa wiki ijayo na Fabregas, ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Hispania kilichotolewa kwenye makundi Kombe la Dunia, anatarajiwa kwenda kukutana na wachezaji wenake kwa mara ya kwanza.
Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal ametua Stamford Bridge kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 30 kutoka klabu iliyomkuza kisoka, Barcelona.
Timu ya Jose Mourinho itaanzia msimu mpya ugenini kwa kucheza na Burnley iliyopanda msimu huu, Agosti 16 kabla ya kuwakaribisha wageni wengine wa Ligi Kuu, Leicester City, Uwanja wa Stamford Bridge wikiendi itakayofuatia.
Wachezaji wengi ambao timu zao zimefanya vibaya Kombe la Dunia, kwa sasa wapo bize na wapenzi wao- na awali BIN ZUBEIRY ilichapisha habari kama hizi juu ya Mario Balotelli wa Italia na Cristiano Ronaldo wa Ureno