MSANII mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kwamba ataolewa endapo somo wake ambaye ni mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse atamruhusu.
Akistorisha na paparazi wetu, Bi Mwenda alisema ruhusa ya yeye kuolewa tena atatoa Maimartha kwani ndiye somo wake hivyo siku atakayotoa ruhusa ataolewa japokuwa hajui ataolewa na nani maana hana mchumba.“Maimatha ndiye somo wangu namsubiria atoe ruhusa ya mimi kuolewa na akishatoa ndiyo nitajua nitaolewa na nani maana sina hata mchumba,” alisema Bi Mwenda ambaye alifiwa na mumewe Salum Mbegu, mwaka 2013.