Marehemu Mwajuma Hamisi Lissu Enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kusikitisha inadaiwa linahusishwa na ugomvi baada ya mama huyo kuachana na ulokole na kujiunga tena katika dini yake ya zamani ya Kiislamu.Akisimulia mazingira ya tukio hilo, mtoto wa pili wa mama huyo ambaye hivi sasa ni marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Charity Jikole alikuwa na haya ya kusema:
Picha ikionyesha sehemu ya ndani ya nyumba ilivyoteketea kwa moto.
“Mama amelipuliwa na petroli. Baada ya moto huo kulipuka chumbani tulikuta nyavu za kwenye dirisha la chumba alicholala zimekatwa, tunaamini mlipuaji ndiye aliyekata nyavu hizo na kupitishia petroli.
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.
Mtoto wa Marehemu, Charity Jikole.
“Mkasa huu unatokana na ukweli kuwa mama yangu awali alikuwa Muislamu lakini kutokana na matatizo yake ya kiafya alishauriwa na baadhi ya watu kujiunga na maombi katika makanisa ya kilokole ili awe anaombewa tatizo la presha.
“Baada ya kushauriwa aliamua kujiunga na makanisa hayo ya kilokole akiamini kuwa angeweza kupona.
“Baada ya kushauriwa aliamua kujiunga na makanisa hayo ya kilokole akiamini kuwa angeweza kupona.
Waombolezaji wakishusha mwili wa marehemu kwenye gari kwa ajili ya mazishi.
“Mama alikuwa ni mjane mwenye watoto watatu na baada ya kujiunga na walokole amekuwa akisali katika makanisa manne tofauti.“Sisi kama familia tunawatuhumu walokole kwa sababu hata baada ya moto huo, baadhi yao hawakuja kusaidia kuuzima wala kutoa maji.
Nyumba ya marehemu inayodaiwa kuteketea kwa moto eneo la Kibamba Hondogo
“Kwa kweli tulishangazwa na kitendo hicho na kuwaona ni watu wabaya sana kwetu.”Hata hivyo, mtoto huyo alisema kifo cha mama yake kimekuja siku moja baada ya kufanyiwa sherehe ya kutoka katika dini ya kilokole na kurudi kwenye Uislamu.
Mchungaji aliyetajwa kwa jina la George Said ambaye anawaongoza walokole wa eneo hilo, alipohojiwa na waandishi wetu alikiri kusikia tuhuma hizo.“Hata mimi nimesikia tuhuma hizo lakini si za kweli hata kidogo na mpaka sasa sijahojiwa na mtu yeyote au hata polisi kuhusiana na tatizo hilo,” alisema mchungaji huyo.
Uwazi lilipompigia simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP, Camillus Wambura na kumuuliza juu ya tukio hilo, alikiri kutokea na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo chake