MKONGWE kwenye kilinge cha sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amewataka mashabiki wake wajue kwamba, muda ukifika wa kupata mume wa kufunga naye ndoa, atafanya hivyo lakini kwa sasa anatoa kipaumbele kwenye kazi tu.
Akizungumza na Amani, Johari ambaye umri wake upo juu ya miaka 30, alisema watu wengi wanafikiri kuwa ndoa ndiyo kila kitu katika maisha lakini kwa upande wake bado hajaifikiria.
“Kitu ambacho nakiamini mimi ni kwamba ndoa kama nimepangiwa na Mungu ipo na itaendelea kuwepo haijalishi hata kama nitafikisha miaka hamsini,” alisema Johari.