M-Net na Endemol Afrika kusini wanayofuraha kuthibitisha upatikanaji wa nyumba mpya ya Big Brother katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini baada ya moto mkubwa kuteketeza nyumba iliyokuwa itumike mnamo tarehe 2 mwezi wa 9 . Utafutaji wa nyumba mpya ulifanikiwa baada ya kuhangaika kutafuta nchini humo na nje ya nchi kwa nyumba itakayofaa kufanyia msimu wa 9 wa show kubwa kabisa Afrika.
M-Net na Endemol Afrika kusini wanafuraha kutangaza kwamba Big Brother Hotshots itaanza siku ya jumapili , Tarehe 05 mwezi wa kumi saa moja kamili.