Monday, September 8, 2014

TAZAMA PICHA ZA SERENGETI FIESTA ILIVYOKUWA HUKO MUSOMA ILIKUWA NI SHIDAAAA

7Asante kwa kila mtu wangu ambae alijitokeza kwenye hii show ya Serengeti Fiesta September 7 2014 Musoma, show ambayo ilifanywa maalum baada ya maamuzi kufikiwa ili upendo usambazwe kwa wote waliofiwa na waliojeruhiwa kwenye ajali ya Mabasi iliyoua 39 Musoma September 5 2014.
Show ilikua ifanyike Ijumaa lakini iliahirishwa siku hiyohiyo baada ya ajali kutokea na ilikua isifanyike moja kwa moja, Jumamosi watu ikiwa ni pamoja na Wasanii wakiwa wamejiandaa na safari, stage kianza kuondolewa ili kusafirishwa…. likaja wazo kwamba inaweza kufanyika show ya Fiesta lakini ikawa maalum kwa ajili ya ajali ya Ijumaa.
Matangazo yalianza kuruka Jumamosi jioni na Jumapili ambapo kiukweli hatuna budi kuwashukuru watu wote waliojitokeza kutoka hata nje ya Musoma na kuja kwenye Fiesta Jumapili hii iliyofanyiwa kazi na Christian Bella, Nay wa Mitego, Chege na Temba, Stamina, Nikki wa II, Young Killer, Shilole, Recho, Roma Mkatoliki na wengine waliokubali malipo yao yakatwe na yapelekwe tena kutoa msaada kwa mara ya tatu hospitali siku ya Jumatatu.
6
2
3
4
5
10
9
11
12
8
14
13
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
Wasanii waliwasha mishumaa mwishoni mwa show na wote wakapanda kwenye stage kama ishara ya kuwakumbuka wote 39 waliopoteza maisha kwenye ajali ya Ijumaa Musoma.
Dj Fetty aliwaongoza wakazi wa Musoma kuimba single ya ‘Kamanda’ wakati wa kuwakumbuka wote waliofariki kwenye ajali ya Ijumaa Musoma.