Wednesday, October 15, 2014

BAADA YA KUPIGWA CHINI NA BABA MTOTO WAKE|:ROSE NDAUKA AFUNGUKA HIVI

 
SIKU chache baada ya uchumba wake kuvunjika, msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka amefunguka na kusema kuwa kwa sasa haitaji tena mwanaume kwani anajikita zaidi katika kufanya kazi.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Rose alisema katika maisha yake ya uchumba alijifunza mambo mengi na anamshukuru Mungu amempa zawadi ya mtoto hivyo anafanya kazi kwa bidii ili aweze kumlea mwanaye vizuri.

Alisema hajutii kwa yaliyomtokea kwa mchumba wake Malik Bandawe, kwani makosa yaliumbwa makusudi ili watu wapate kujifunza, hivyo akili yake kwa sasa anaiwekeza katika kazi zake za sanaa.